WALEMAVU WANAPASWA KUTHAMINIWA...!!!!
Tumefanikiwa kuangaza Vijijini na
kutembelea katika Shule ya Walemavu ka Katumba 2 iliyopo Wilaya ya
Rungwe, Mkoani Mbeya, jamani wanahitaji msaada ili nao wajione wana nafasi
na mchango mkubwa wenye umuhimu katika jamii.
Sio kuwatenga, sio kuwaacha kwani sote ni sawa, kumbuka kuwa nao wanandoto kuwa kama huyu au yule.
Wasaidie kwa moyo wako wote watoto hawa.
Sote
yatupasa kuwa nao, tushirikiane kwa pamoja tuhakikishe nao pia wanapata
elimu ya kutosha. (Picha na Kamanga na Matukio & Chimbuko Letu,
Katumba - Mbeya)
******
Makala na Ester Macha, Mbeya.
Walemavu ni watu ambao wanatakiwa kuthaminiwa
katika jamii
kutokana na hali halisi ya maumbile yao
waliyozaliwa nayo au hata kwa waliopata ulemavu baada ya kuzaliwa kuwa hivyo jamii hiyo haina budi kupewa kipaumbele
katika masuala muhimu hususani suala la elimu ambapo wengi wao wamekuwa
nyuma kielimu.
Nadiriki kusema hivyo kwasababu mara nyingi jamii imekuwa
ikiwasahau walemavu na kuwatenga kutokana na jinsi walivyo na kusahau kuwa nao
wana haki ya kuheshimiwa, kupendwa, kuthaminiwa kama
watu wengine ambavyo wanajaliwa na
jamii.
Lakini cha kushangaza hali hiyo imekuwa tofauti kwa jamii
hii ya walemavu ambapo baadhi ya kaya zimekuwa zikiwatenga watu hawa kwa
kuwafungia ndani kwa kuona kuwa ni mkosi katika familia husika.
Vile vile hata wabunge na madiwani wamekuwa wakisahau jukumu la kuwasaidia walemavu na kujikuta
wakiendelea kusaidia wananchi wengine huku wakifahamu kuwa kuna kundi lingine
la walemavu ambao wanahitaji msaada mkubwa hasa maeneo ya vijijini ambako
wamekuwa na dhana ya kuona kuwa walemavu ni mkosi katika familia zao.
Nashauri viongozi waliopewa mamlaka ya kusaidia wananchi pia
waone au kufika vijijini na kutambua kero mbali za walemavu na si kuwaangalia
watu wanaojiweza pekee yao
ambao ndio wameona ni msaada pekee kwao.
Huko vijijini kuna walemavu wapo ndani zaidi ya miaka 20
hawajawahi kutoka nje zaidi ya kukaa ndani tu, kama
viongozi hawataweza kujua kero za wapiga wao kwa kuangalia pande zote mbili
ambazo ni walemavu na wananchi wenye uwezo huku wakisahau kundi hili la
walemavu ambao nao ni wapiga kura licha ya kuwa ni walemavu.
Katika pita pita yangu nimekuwa nikishuhudia mikutano au
vikao vingi ambavyo vimekuwa vikifanywa na Wabunge na Madiwani lakini kilichonisahangaza sijaona kati ya
viongozi hawa aliyejaribu kugusia kero za walemavu ambazo zinawakabili katika
maeneo yao.
Jambo ambalo nimeliona na ambalo linatakiwa kuigwa na
wabunge na madiwani wengine ni hili la
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw.Philipo Mulugo (Mb) kuweka
kipaumbele kwa walemavu na wazee ambao hawajiwezi kimaisha kuwasaidia kila
anapofika kufanya mikutano ya hadhara katika Jimbo lake yote ni kuweza kujua kero za wananchi wote.
Nimeamua kusema hivi si kwamba nimeamua kumpa sifa Mbunge
huyu bali ni kutokana na utendaji wa kazi wake wa Ubunge ambao amekuwa
akiufanya bila ubaguzi kwa kuona kuwa kuna kundi maalumu la walemavu wote ambao
wanastahili kupata huduma na kama watu
wengine.
Kwa kutambua kundi hili mbalo mara nyingi limekuwa
likitengwa na jamii na hata wengine
wameshindwa kutoka ndani zaidi ya miaka
20 sasa Bw. Mulugo aliamua kutoa baiskeli 200
zenye thamani ya mil. 50 kwa walemavu na wazee wote wa jimbo lake la Songwe .
Ninachokiona hapa ni kwamba
Mbunge huyu aliamua kufanya hivi baada ya kuona kuwa jimbo hilo la
Songwe kuwa na idadi kubwa ya walemavu ambao hawakuwa na msaada wowote na kuona
umuhimu wa kuwasaidia wale walemavu ambao hawajaweza kutoka ndani kwa muda
mrefu kutokana na hali halisi waliyonayo.
Si jimbo la songwe pekee lenye walemavu bali hata majimbo mengine pia yana
walemavu wengi ambao wanahitaji vitendea kazi ili waweze kutembea na
kufanya shughuli zao je nani wa kuwaona kama
si viongozi wenyewe kuangalia makundi haya ambayo mara kadhaa yamekuwa yakitengwa na jamii?
Nimekuwa nikishuhudia idadi kubwa ya walemavu wakiwa mitaani
kuomba kuomba ili kuweza kujikimu kimaisha kutokana na hali duni waliyonayo ya
kimaisha.
Nionavyo kwa upeo wangu msaada huu hautoshi pekee bali
kinachotakiwa ni kupata nguvu nyingine ya kuwasaidia walemavu ili nao waweze kujisaidia wenyewe kwa nguvu
zao kwa kuwa wamepata vifaa mbavyo vitawawezesha kuweza kushiriki vema shughuli
zote za kijamii.
Si kwamba napinga msaada wa Bw. Mulugo kwanza napongeza kwa
wazo zuri alilokaa na kufikiri kwamba kundi hili limekuwa likihitaji msaada
mkubwa na pia ameona mbali kwa kuona kuwa walemavu mara nyingi ni watu ambao
wanakuwa watengwa na jamii na hata viongozi walio wengi wamekuwa wakiwasahau kwa
mchango wao.
Ushauri wangu kwa Bw.Mulugo ni kuongeza bidii zaidi kwa
kutafuta mbinu mbali mbali za kuweza kuwsaidia walemavu wa jimbo lake ambao kwa
sasa
wamepata miguu ya kutembelea kikubwa kilichopo kwao ni Mbunge huyu
kuwatafutia mitaji ili waweze kufanya shughuli zao wenyewe na si kukaa
kutegemea
kupata misaada.
Pia jamii nzima kwa ujumla tukiwa na mitazamo ya namna hii tutaweza kuwawezesha walemavu Tanzania kujikwamua katika umasikini uliopindukia
na walemavu waliofichwa majumbani waweze kutolewa
na walemavu waliofichwa majumbani waweze kutolewa
nje na kusaidiwa kwa kufanya hivyo
kutafanya idadi ya walemavu wanaofichwa ndani kupungua na hata wale ambao
walikuwa hawatembei wataanza kujishughulisha ili kujiongezea vipato na hatimaye kuacha kuwa tegemezi.
Comments
Post a Comment