WATOTO WA MITAANI WANASWA KITUO KIKUU CHA MABASI UBUNGO, WAFIKISHWA MAHAKAMANI DAR-ES-SALAAM

Watoto wa mitaani wakipelekwa kwenye gereza la watoto lililopo Kisutu jijini Dar es Salaam.
WATOTO wa mitaani  leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Sokoine Drive jijini Dar na kufunguliwa mashitaka ya uzururaji. Watoto hao walinaswa kwenye msako uliofanyika kwenye kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani ‘Ubungo Bus Terminal’.
Pichani juu ni baadhi ya picha za watoto hao na yeyote anayetaka kujua zaidi kuhusu watoto hao, afike kwenye gereza la watoto lililopo Kisutu.  Majina yao yapo kwenye karatasi hapo juu.  

SERIKALI ITAFUTE NJIA MBADALA YA KUWASAIDIA HAWA WATOTO, HII KAMATAKAMATA SIO SULUHISHO LA KUONDOKANA NA WATOTO WA MITAANI NA OMBAOMBA KWA UJUMLA, KUTOKANA NA FURSA TULIZONAZO NCHINI NI VEMA SERIKALI IKATENGA ENEO MAALUMU KWA AJILI YA HAWA WATOTO, PIA SERIKALI IWAWEZESHE KWA NAMNA AMBAYO ITAWAFANYA WAONDOKANE NA UTEGEMEZI NA KUOMBAOMBA, KWA MFANO WALE WENYE VIPAJI KUWAENDELEZA KATIKA VIPAJI VYAO NA WENGINE WAPEWE NYEZO ZA KUJITEGEMEA KAMA VILE UFUNDI AU HATA KILIMO NA UFUGAJI. 

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU