“”””””””””HAKUNA UGUMU WOWOTE KUFUNDISHA WATOTO VIZIWI “ Asema
mwalimu-mwanafunzi Madeghesho Fabiola.
Watu wengi huwa na notion kwamba kufundisha watoto
viziwi ni kitu kigumu sana hasa ukizingatia kuwa wanahitaji lugha ya alama
kufundishiwa, kwa mwalimu Fabiola anaona si changamoto kubwa kama tunavyofikiri
hivyo kuwaasa waalimu wengine wasiogope kujifunza lugha ya alama ili kuwasaidia
watoto hawa.
Mwalimu Fabiola ambaye
anachukua shahada ya awali ya elimu maalumu kitengo cha viziwi katika chuo cha
kumbukumbu cha Sebastian Kolowa kilichopo Lushoto mkoani Tanga, ameyasema haya baada ya kumaliza
mafunzo ya vitendo (field) aliyokuwa akiyafanya katika shule ya msingi Meru
iliyopo mkoani Arusha, ambayo shule hiyo imeambatana na kitengo cha viziwi.
Mwalimu huyo aliongeza
kuwa “Nimejisikia
fahari kubwa sana kuweza kuwasiliana na watoto hawa na kuelewana nao vizuri, ni
watoto ambao kwa kweli wanafundishika na wana shauku kubwa ya kujua vitu vingi,
hilo limenifurahisha sana na kunipa moyo wa kuisoma lugha ya alama ipasavyo ili
pindi nimalizapo shahada yangu nijikite kuwasaidia watoto hawa.”
Aidha mwalimu huyo
ameiomba wizara ya elimu kuweka mitaala ambayo itawawezesha wanafunzi wotewanaosikia
na wasiosikia kusoma lugha ya alama kama somo ili waweze kuwasaidia wanafunzi
wasiosikia wakiwa ndani ama nje ya shule ili kupelekea elimu jumuishi kushamiri katika nchi yetu na amewaasa waalimu
kutoiangalia taaluma ya elimu maalumu kama si muhimu kwa taifa letu na
kumalizia kuwa watoto walemavu ni jukumu letu sote kuwaangalia na kuwapa mwanga
wa maisha yao.
Mwalimu Fabiola akiwa na wanafunzi viziwi Shule ya msingi Meru ArushaMwanafunzi Naomi akiwa katika pozi mara baada ya kufundishwa na mwl. Fabiola
Mwanafunzi Mukhsin katika pozi
Wanafunzi wa darasa la pili katika picha ya pamoja
Comments
Post a Comment