'''LIFE WITHOUT LIMIT'''

Nick Vijicic alizaliwa 1982 Mwezi wa kumi na mbili, huko Serbian Melbourne, Astralia kama mlemavu asiyekuwa na miguu wala mikono,mwili wake upo kama nusu mtu. Siku alipozaliwa wazazi wake walilalamika sana na muda mwingine walijuta kumzaa mtoto huyo, hata katika kanisa alilokuwa akiongoza Baba yake lilimtatiza sana kiasi ambacho alikosa raha ya kutetea yaliyotokea kutokana na imani aliyokuwa nayo.
                                                 Nick Vijicic.

Wazazi wa Nick walikuwa wakijuta kila siku na hata kutubu kwa Mungu kwa kudhani wamemkosea Mungu kuwaletea mtoto huyo.Walijiuliza kwa nini imetokea? Na nikosa la nani? Na walikuta kuwa si madaktari wala mimba ya mama yake kama kosa la kusababisha kuwa jinsi alivyo.

[nick_vujicic_03.jpg]

Maisha yakiwa magumu,katika ugumu wa kuishi,serikali ya Astralia ilizuia kwa watoto walemavu kuchanganywa na wale wasio walemavu lakini baadae serikali ilikuja kubadili sheria hiyo,kisha Nick alianza kusoma pamoja na wenzake.

                          Nick akiwa darasani enzii za udogo wake.

Nick alipigana kwa kuamini kuwa anaweza na akaweza, na akafanikiwa kuwa Mkurugenzi wa LIFE WHITHOUT LIMBS, Taasisi ya kuhamasisha mafanikio kwa watu walemavu na wengine wa kawaida. Watu wengi walimuonea huruma nakusema kwa nini Mungu alimuumba binadamu huyu katika mazingira magumu kama hayo?

Lakini yeye aliamini kuwa hana mipaka katika maisha yake ,akatunga kitabu chake kiitwacho "Maisha Bila Miguu,Bila Mikono,Bila Wasiwasi''na kutoa DVD yake iitwayo "Dhumuni Langu kubwa Maishani"

Nabaadae akafanyikiwa kuanzisha kampuni iitwayo "Attitude Is Attitude"

Moja ya Mialiko mikubwa anayo pewa Nick kubadili fikra za watu wenye kukata tamaa ya kuishi kutokana na ulemavu au ugumu wa Maisha.
Akibebwa na wanafunzi wa nchi ya Afrika kusini.

Nick alipigana katika vita ya Maisha ,hakuangalia mapungufu ya mwilini bali alijua kuwa yeye ni zaidi ya jinsi alivyo,alipigana kiakili,kisaikolojia,kifikra toka enzi zake za utoto,ujana utu uzima na zaidi alikuwa akijiuliza dhumuni la maisha yake hapa na alisema tena maneno haya.

NUKUU- Mimi ni zaidi ya jinsi nilivyo,nataka na wewe ujisikie hivyo,haijalishi unapitia maisha gani na maumivu gani.Mwisho wa kunukuu.

Zaidi Nick aliweza kutunga kitabu kiitwacho maisha bila mipaka {"Life Without Limit"}Sijui wewe unapitia shida gani,lakini jikubali natambua wewe ni zaidi ya jinsi ulivyo.

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU