WATOTO WALEMAVU WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA HUDUMA ZAO SHULENI


Na Fabiola Nassib wa HEAR MY VOICE-Arusha
Watoto wenye walemavu waishio mkoani Arusha wameililia serikali juu ya
kuboresha mfumo wa elimu hasa sekondari unaowatenga hali inayowafanya
kukata tamaa ya kuthamini elimu.
Wakiongea na HEAR MY VOICE ilipotembelea shule ya msingi Meru kwa
niaba ya wanafunzi wenzake wenye ulemavu wa aina tofauti tofauti
Brenda Honest mwenye ulemavu wa kutosikia (KIZIWI) alisema kuwa  mfumo wa elimu
hasa wa shule za sekondari hauwajali wala kuthamini walemavu kama wao.
Brenda aliendelea kusema kusema kuwa ingawa wao ni walemavu lakini jamii
itambue kuwa ulemavu huo hawakuuchagua hivyo ameiomba serikali na
jamii yote kwa ujumla kuwasaidia kwa kuwasapoti katika mambo mbali
mbali zitakazowawezesha kujitegemea hapo baadae na siyo kuwa tegemezi
siku zote za maisha yao.
Akitolea mfano mambo wanayohitaji kuungwa mkono Brenda alisema kuwa
mfumo wa elimu hasa katika shule za sekondari na kuendelea, haijawapa
kipaumbele walemavu hasa wa kusikia, kuona, wenye mtindio wa ubongo
n.k kwa uboresheji vifaa vya kufundishiwa, walimu maalum kwa ajili yao
pamoja na punguzo la ada hali itakayowafanya kupata moyo wa kusoma.

“kutokana na hayo basi, sisi walemavu tunalia na serikali kwa
kuendelea kututengenezea mazingira ya sisi tuendelee kuwa watu
tegemezi badala ya kujitegemea wenyewe kiuchumi hapo baadaye kwani
kuna wenzetu wengi tu wamefundishwa vizuri shuleni hapa walipoenda
secondari wakashindwa masomo na kukata tamaa baada ya kuona hawaelewi
masomo lakini wanaendelea kusogeza madarasa” alisema Brenda
“Mbali na kuililia serikali kupewa upendeleo wa kielimu, pia sisi
walemavu wasichana mashindano mengi ya kitaifa tumekuwa tukishuhudia
kwa wenzetu tu lakini sisi hatushirikishwi hali inayotufanya kujiona
tumetengwa zaidi hivyo nitumie nafasi hii kuiomba serikali itambue
mchango wa walemavu kiuchumi, kijamii, na hata kisiasa pindi
tunapopiga kura kuwaweke madarakani”alimalizia Brenda.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo ya msingi Meru, ambaye pia
ni mlezi mkuu wa watoto walemavu wawapo shuleni Bwana Mussa Luwambano
alisema kuwa katika shule Meru wana watoto 76 wenye ulemavu tafauti
tofauti ambapo hafundishwa zaidi ya miaka saba ikilinganishwa na
wenzao wasio walemavu.
Akielezea changamoto kubwa wanayokumbana nazo katika kuwawezesha wenye
ulemavu kupata elimu itakayowasaidia katika maisha yao hapo baadae
katika kujitegemea Luwambano alisema kuwa ni ukosefu wa vifaa vya
kufundishia pamoja na usafiri maalum hali ambayowalemavu wamekuwa
wakichelewa shule sambamba na baadhi yao kupoteza maisha kwa kugongwa
na magari hasa viziwi wasiosikia milio wala honi za magari.
Pia aliongeza kuwa mbali na hilo pia mfumo wa elimu ya walemavu
haujajizatiti katika elimu ya sekondari kwa kuwepo na walimu maalum wa
kuwafundusha, madarasa, vifaa na hata miundo mbinu kwa ujumla hali
inayosababisha baadhi ya watoto kuishia elimu ya msingi na kuendelea
kuwa tegemezi kwa zinowazunguka kitendo ambacho ni kikwazo kikubwa kwa
uchumi wa nchi yetu.
“Baada ya kuona watoto wengi tunaowafundisha wakifaulu kwenda
sekondari hurudi kwa kushindwa masomo, tumeamua kuwajengea chuo cha
ufundi ili wamalizapo elimu ya msingi angalau wajiendeleze kiufundi,
hivyo serikali hasa halmashauri yetu ya jiji la Arusha , taasisi
,mashirika na watu binafsi wajitokeze kuisaidia chuo hicho kukamilika
ili watoto hawa wajiendeleze kiufundi kuliko kubaki mitaani na kuwa
ombaomba”Alisema mwalimu Luwambano.
Aidha pia mwalimu Luwambano aliwataka wananchi kutambua kuwa malezi ya
watoto ni jukumu kila mmoja wetu bila kujali ni mlemavu au laa hivyo
wajitokeze kuwasaidia pindi wawaonapo wamepata shida hasa wakiwa
barabarani wawavushe kuepusha kugongwa na magari.

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU