Jamii inapaswa kutambua na kuweka mazingira sahihi kwa ajili ya Walemavu (835) Views ULEMAVU ni athari ya muda mfupi au ya kudumu inayosababishwa na hitilafu za kiwiliwili au hisia mfano uoni, usikivu, akili, kusema na kumsababishia mtu kushindwa kufanya kazi kikawaida. Jamii ya watu wenye ulemavu nchini ni kundi kubwa miongoni mwa takribani ya watanzania milioni 45, ambao wamesahaulika katika sekta mbalimbali kutokana na jamii kuwatenga na kusahaulika kabisa bila kuwasaidia katika maisha ya kila siku. Kwa miaka mingi, suala la ulemavu halikupewa umuhimu na uzito wowote katika jamii kutokana na mitizamo na imani potofu. Kuna aina nyingi za ulemavu, kuna ulemavu wa viungo, ulemavu wa uoni, kiziwi na matatizo ya kusema, ulemavu wa akili, albino (ulemavu wa ngozi) mwingineo kama kifafa, kichwa kikubwa mpasuko wa mdomo pamoja na ulemavu mchanganyiko ambapo mtu anakuwa na ulemavu zaidi ya mmoja katika jamii tunayoishi. Wahenga walinena kuwa “hujafa hu...
Comments
Post a Comment