TUWASADIE WATOTO YATIMA NA WATOTO WA MITAANI
Hiki ndicho kitanda cha mtoto huyu
Kwa watoto hawa popote ni kitanda
Wapo watoto wengi ambao wanaishi maisha ya shida na taabu nyingi, wengi
wakiwa wameondokewa na wazazi wao (wamefiwa na wazazi wao). Ni kweli
kuwa serikali ina jukumu la kuwaangalia watoto hawa. Sisi
wanajamii pia tuna majukumu ya kuwasaidia watoto hawa. Tukijitahidi
kupunguza matumizi ya anasa tukachangia kila mwenye uwezo kidogo kidogo
hata elfu moja kwa mwezi kwa wale walioajiriwa na hata wafanyabiashara
tungeweze kutatua tatizo hili tukishirikiana na serikali. Kuna vituo
vingi vinavyolea hawa watoto ila vinakosa uungwaji mkono kutoka kwa
wanajamii, kwa hicho kidogo ulichojaliwa na Mungu unaweza okoa maisha ya
mtoto walau mmoja. Mother Teresa alipata kusema "Kama huwezi kusaidia
mamia ya watu, saidia hata mmoja"
Naamini jambo hili linawezekana kwa wote wenye imani na uchungu. Fikiri, Chukua hatua, Inawezekana.
Naamini jambo hili linawezekana kwa wote wenye imani na uchungu. Fikiri, Chukua hatua, Inawezekana.
Comments
Post a Comment