NI WAJIBU WETU.
JAMII IWAJIBIKE KUWASAIDIA WATOTO WA MITAANI, YATIMA....
Kitanda usichokilalia, huwezi kujua
kunguni wake, shida na mateso wanayoyapata watoto waishio katika
mazingira hatarishi na wale wa mitaani ni vigumu kuyaeleza. Watoto hawa
hawajui leo au kesho watakula nini, hakuna anayehangaika kuwatafutia
chakula, wanapolala na njaa hakuna wa kumlilia na wakiumwa hakuna wa
kumweleza hivyo huendelea na maisha yao hadi wanapopata nafuu au kupona
kabisa.
Ukweli ni kwamba, watoto hawa
hujisikia wapweke kutokana na jamii kubwa kuwakataa na kuwaweka katika
fungu tofauti. Jambo la kusikitisha ni idadi kubwa ya watoto hawa umri wao
unaanzia miaka miwili hadi kumi ambao kimsingi hawajui kujitegemea, njaa
ikiuma wanalia tu na kushindwa kujieleza. Kitanda chao ni barabarani na
wengine mitaroni, baridi yote ya usiku na jua la mchana ni lao ,hawajui
kubadilisha nguo, zile walizovaa wiki iliyopita hadi leo hazijatoka
mwilini, Tumezoea kuwaona watoto wenye wazazi wakitoka nyumbani
asubuhi na kurudi majumbani mwao jioni. Watoto yatima na wanaoishi
katika mazingira hatarishi hawana pa kwenda, popote wanalala. Jamii
imesahau kuwa watoto hawa ni sawa na wao, wanasikia njaa, baridi na
maumivu sawa na wenzao lakini nani anashughulika nao?
Watoto hawa hawakuchagua kuwa
yatima na kuishi mitaani, hawakuchagua kufiwa na wazazi wao, wamejikuta
wapo mitaani na hawana la kufanya kama watoto wetu wanavyojikuta wakiwa
mikononi mwetu na wanapata kila kitu. Waswahili wanasema, kinga ni bora
kiliko tiba. Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs na yale ya kimataifa
kama UNICEF na Serikali ,wanashughulikia tatizo la watoto hawa wakiwa
tayari mitaani, jambo ambalo ni sahihi na la msingi, ni bora nguvu inayotumika kuwasaidia watoto
hawa ingepaswa kuelekezwa kwenye kinga ili kutibu tatizo hilo
kabisa. Sababu moja wapo inayochangia ongezeko la yatima na watoto wa
mitaani ni migogoro isiyokwisha katika ndoa na umasikini uliokithiri
Hatua za haraka zinahitajika
ili kupunguza au kumaliza tatizo la watoto wa mitaani na yatima kwa
kuwaunganisha na walezi pamoja na ndugu zao ambao tunaamini wapi.
Umefika wakati wa serikali
kuratibu nguvu za NGOs kwa kuhakikisha mashirika hayo na jamii wanachukua hatua stahiki kuhakikisha tatizo hilo nchini
linakwisha...
MUNGU IBARIKI TANZANIA... MUNGU IBARIKI AFRIKA.
dunia haina usawa, wengine wana maisha mazuri ili hali wengine mlo mmoja kwao ni taabu
ReplyDeleteNi kweli kabisa na kitu kikubwa kinachosababisha yaho yote in UBINAFISI.
DeleteNi kweli kabisa na kitu kikubwa kinachosababisha hayo yote in UBINAFISI.
Deletemtu anakuwa na gari 20 za kutembelea, anakutana na watoto wa mitaani hata kuguswa tu na hali waliyonayo wale watoto kwake haipo.
DeleteInabidi roho mtakatifu atuguse katika hili.
Delete