ATELEKEZA FAMILIA KISA MKE KAZAA WATOTO WANAOFANANA NA NYANI.
Mwanaharusi Juma akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake Ahaj (10) mwenye shati Nyekundu na Abdulatifu.
Abdulatifu Sadik (5) akipata kifungua kinywa nje ya nyumbani kwao.
Mtoto Alhaj akiwa amesimama.
Mtoto Alhaj akiwa anatembea.
Mtoto Alhaj. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Mjumbe
 wa kamati ya shule ya msingi Ndulungu tarafa ya Ndago wilayani Iramba 
mkoa wa Singida, Sadik Suleman Mnyawi (44), amemtelekeza mke wake mdogo 
Mwanaharusi Juma (34), kwa zaidi ya miaka miwili na kumsababishia maisha
 kuwa magumu.
Imedaiwa kwamba Mnyawi amemtelekeza mke wake huyo, kwa madai kwamba amezaa watoto wawili wanaofafana na nyani.
Mjumbe
 huyo wa kamati ya shule, amemtelekeza mke wake mdogo na kumpora nguo 
zote na kumwachia zile alizokuwa amevaa tu.  Pia aliondoka na matandiko 
yote ya kitandani na kubakisha chaga pekee.
Akizungumza
 na waandishi wa habari, Mwanaharusi awali alikuwa ameolewa na mwanaume 
mwingine waliobahatika kupata mtoto mmoja, Fadhili Juma (15).
Alisema
 baada ya kuachana na mwanaume wa kwanza, mwaka 2002, aliolewa na Mnyawi
 ambaye amemtoroka na kumwacha bila matunzo yoyote ya watoto watatu 
aliozaa naye.
Alisema
 katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yake na Mnyawi, walifanikiwa kupata
 watoto watatu kati yao, wawili wakiwa wanafanana na nyani.
 “Mtoto
 wangu yule niliyezaa na mume wa kwanza, Fadhila Juma, yeye yupo darasa 
la saba mwaka huu.  Ramadhani  (6) ambaye nimezaa na Mnyawi, yeye 
anasoma darasa la kwanza hapa Ndulungu”,alisema.
Mwanaharusi
 alisema kwa watoto wake aliozaa na Mnaywi,Alhaj (10) na Abdulatifu (5) 
ambao wana sura ya mnyama kutokana na hali zao zilivyo, wameshindwa 
kuanza  shule.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao wanaofanana na nyani, hawasikii wala hawasemi.  Mawasiliano yao yanategemea  ishara tu.
“Ukiacha
 matatizo yao ya kutokusikia na kuzungumza, pia wanahema kwa tabu 
kubwa.  Kama huwaoni, ukisikia wanavyohema, unaweza ukafikiria kwamba 
hao zio binadamu ni nguruwe anahema”,alisema kwa masikitiko.
 Mwanaharusi
 alisema mikono yao ni midogo mno na mifupi na ni dhaifu, matumbo na 
macho yao ni makubwa.  Alhaji pekee ndiye mwenye uwezo wa kusimama na 
kutembea umbali mfupi na mwenendo wake unafanana na wa nyani.
Hata
 hivyo, alisema watoto hao wawili aliwazaa wakiwa wana sura za binadamu 
na afya zao zikiwa njema kabisa.  Lakini wakati wanaendelea kukua, ndipo
 walipoanza kuugua mara kwa mara na kisha kubadilika sura.
“Wakati
 bado tunaelewana na mume wangu, tuliwahi kumpeleka Alhaji katika 
hospitali ya mkoa wa Singida.  Alichunguzwa na  alibainika kuwa na 
upungufu wa damu.  Aliongezewa damu na kisha tuliruhusiwa kurudi 
nyumbani”,alisema.
Alisema
 baada ya kurudi nyumbani, haikuchukua muda, Alhaji alianza kuugua tena 
na baada ya kumshawishi mume wake Mnyawi, wampeleke hospitali ya rufaa, 
ndipo alipomkimbia na kuhamia kwa mke wake mkubwa.
Akizungumza
 kwa masikitiko makubwa,alisema kuanzia wakati huo, anaishi maisha 
magumu mno ambayo ni ya kuomba omba.  Mnyawi pamoja na familia yake, 
amewabembeleza wamsaidie mizigo wa kuwalea watoto hao, wamegoma kabisa.
Kwa
 upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho, Idd Nyauli, alisema 
wamejitahidi kumshauri Mnyawi amrudie mke wake mdogo ili waweze kuwalea 
watoto wao pamaja,  jitahida hizo zimegonga mwamba baada ya Mnyawi 
kugoma kumrudia Mwanaharusi.
Naye
 mratibu elimu wa kata hiyo Mwekwa Mwekwa, alisema watoto hao wawili, 
shule inayowafaa ni ile ya watoto wenye mtindio wa ubongo na si hizi za 
kawaida.
Jitihada
 ya kumtafuta Mnyawi ambaye anaishi kijiji hicho cha Ndulungu, hazikuzaa
 matunda baada ya kuelezwa kwamba baada ya kusikia waandishi wa habari 
watafika kijijini hapo, alifunga safari na kuelekea jijini Mwanza.
Comments
Post a Comment