WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA KUWAKABIDHI MISAADA.

 Wafanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha operesheni, wakipozi kwa picha na watoto wanaolelewa katika kituo cha Ijango Zaidia Orphanage cha Sinza walipokwenda kupeleka msaada wa vyakula, sabuni, mafuta ya kupikia na vyandarua ikiwa ni moja ya mikakati ya NBC kurudisha sehemu ya faida waipatayo katika jamii. Hafla ilifanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Wengine ni watumishi wa kituo hicho.

 Mkurugenzi wa Uendeshaji na Huduma wa Benki ya NBC Tanzania, Cornie Loots (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua kwa Mkuu wa kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage , Bi. Zaidia Nuru Hasani, vilivyotolewa na NBC kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.

 Mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, Ramia Mahmoud , akipokea mafuta ya ngozi kwa niaba ya wenzake vyaliyotolewa msaada na Benki ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo, Ernest Paulo Mbepera (kulia) kituoni hapo, Sinza, jijini Dar es Salaam. Benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua.

 Mfanyakazi wa Benki ya NBC, Mwanaisha Nassoro Ayosi (kulia) akikakabidhi misaada iliyotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.

Mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, Amina Twahilu, akipokea moja ya vyandarua kwa niaba ya wenzake vilivyotolewa msaada na Benki ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo, Anyelwisye Enock Mwakatobe (kulia) kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi. Benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia na sabuni. 

Mambo ya kujiuliza kwa wewe Mungu aliyekujalia uwezo wa kila namna ikiwemo Mali, ni mara ngapi umechukua maamzi ya namna hii? Walau kumsaidia mtoto mmoja anayehitaji msaada.? Mother Teresa alipata kusema"If you can't feed a hundred people, then feed just one." hili ni suala ambalo watu wengi tumelisahau na kutothamini kwa namna moja ama nyingine watoto wenye mahitaji maalumu ikiwemo watoto wenye ulemavu, watoto wa mitaani, watoto yatima na watoto wanaotumikishwa kazi ngumu zisizoendana na umri wao. Tena ni kwa makusudi mazima wale wale wenye uwezo mkubwa wa kifedha ambao ndio wanapaswa kwasaidia hawa watoto ndio walewale wanaowatumikisha katika viwanda vyao na katika majumba yao kwa ujira mdogo au hata kuwadhurumu sitahiki yao kwa kazi ngumu wanazofanya. 

Ni walewale wasiowathamini hawa watoto ndio wanaotoa mamilioni ya pesa katika michango ya harusi kwa kushindana na kuoneshana kuwa wana pesa nyingi, hili sio jambo zuri hata kidogo tuwe na UPENDO kwa hawa watoto kwani kwa kufanya hivyo hata MUNGU ambaye ndiye mpaji wa vyote tulivyonavyo atazidi kutuongezea zaidi ya tulivyonavyo. 
ASANTE SANA WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC KWA UPENDO WENU KWA HAWA WATOTO.

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU