ANGALIZO KWA JAMII



‘VITUO MASILAHI BINAFSI VINACHANGIA ONGOZEKO LA WATOTO WA MITAANI ’
KUZAGAA kwa watoto wa mitaani nchini kunaelezwa kuwa kunatokana na vituo vingi vya kuwalea watoto hao kushindwa kuwapatia mahitaji stahiki.
Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mipango na Uendeshaji wa Mfuko wa Kusaidia Watoto wa Mitaani na Yatima (MKUWAMITA), Yohana Mgandi, alipozungumza na Tanzania Daima.
Alisema waliyabaini hayo katika utafiti wao walioufanya katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia mwaka 2004 katika mikoa 19 iliyohusisha wilaya 23 na vijiji 16.
“Kuzagaa kwa watoto wengi wa mitaani kunatokana na vituo vingi kushindwa kuwalea ipasavyo kutokana na wengi wa wanaovianzisha kuangalia masilahi yao binafsi,” alisema Mgandi.
 Katika utafiti uliofanya na uongozi wa HEAR MY VOICE umebaini kuna shule binafsi zinazosajiliwa kwa malengo ya kuwasaidia watoto wenye mahitataji maalumu ila mwisho wa siku malengo hayo yanageuzwa na kuwa biashara ambapo watoto waliokuwa wakipatiwa huduma katika shule hizo wakaanza kurejea mitaani kujitafutia riziki zao za kila siku.
Serikali inapaswa kuwa makini na watu wa namna hii, badala ya kupunguza tatizo kwa ubinafsi wao na uroho wa pesa wanaongeza tatizo katika jamii.
WITO wangu kwa jamii inatupasa kuwa makini na watu wa namna hii, pia hivi vitaasisi vinavyoibuka kila leo, kila kona kwa gia ileile ya kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu viangaliwe kwa makini. Tusigeuze matatizo ya hawa watoto kuwa mtaji wa kujinufaisha pasipo kuwa na nia ya dhati katika kuwasaidia 



Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU