TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanadamu mkamilifu apoamka asubuhi na kuanza siku yake kwa kutekeleza
majukumu yake ya kawaida ya kila siku ya kujiingizia kipato halali cha kujikimu
na kuyafanya maisha yasonge mbele huwa siyo rahisi kukumbuka kuwa kuna binadamu
ambao wanahitaji msaada na uangalizi wa karibu sana.
Mashirika, Taasisi mbalimbali za
serikali na binafsi aidha watu mmoja mmoja katika kuangalia makundi maalum ya
kusaidia mara nyingi huwakumbuka watoto yatima na waishio katika mazingira
magumu, wazee na walemavu wa viungo. Lakini kuna kundi maalum ambalo jamii
hulisahau bila kulipa kipaumbele..
Walemavu wenye utindio wa ubongo
katika jamii zetu za kitanzania husaulika sana na kuachwa bila msaada wowote wa
karibu, mfano kupatiwa huduma ya karibu kama huduma za kiafya, elimu aidha kuwa
na mahusiano ya kawaida katika jamii zetu.
Familia zilizo nyingi pamoja na
jamii zetu akizaliwa mtoto mwenye utindio wa ubongo huonekana kuwa ni mkosi
katika familia jambo ambalo hupelekea mtoto huyo kutengwa au kufichwa ndani au
kujengewa kijumba mbali na familia na kunyimwa haki zake za msingi kama watoto
wengine.
Lakini kutokana na kundi hilo
hitaji kuonekana halina msaada wowote, mfano vituo maalum vya kuwalelea watoto
hao na kuwapatia mahitaji yao maalum ikiwemo
elimu, aidha kutokana kuwa katika jamii watoto hao wapo wengi na hawana msaada
Mama Stephanie Koster aliamua kuanzisha kituo cha kuwalea watoto hao.
Stephanie Koster ni mama wa
Kijerumani ambaye aliliona tatizo hilo
katika mkoa wa Kagera na kuamua kuanzisha kituo cha kuwalea watoto wenye
ulemavu wa mtindio wa ubongo chini ya kanisa Katoriki Jimbo la Bukoba katika
eneo la Kemondo Wilaya ya Bukoba na kituo kinaitwa Mt. Nicholaus.
Mama Koster ana upendo mkubwa na
watoto hao na anajitoa kuwapenda, kuwalea, kuwatunza na kuwapatia huduma za afya na elimu na kuwafanya
watoto hao kujisikia wanadamu kama
wengine kwani mama huyo huwapeleka watoto hao katika shule za karibu za Mubembe
na Bethania.
Mama Koster mama Mjerumani
anasema kituo hicho kiliazishwa na kufunguliwa rasmi tarehe 13.11.2011 na
Mhashamu Askofu Nestory Timanywa Askofu
jimbo la Bukoba wakati huo na kituo hicho kilianza na watoto kumi wakiwa chini
ya mama huyo mlezi na kina uwezo wa watoto 25.
Stephanie Koster anasema
alianzisha kituo hicho ili kuionyesha jamii kuwa watoto hao wana haki sawa na
wengine katika jamii na wazazi wenye watoto hao wanapaswa kuwalea watoto
wenyewe bila ya kuona kuwa huo ni mkosi au kuwatenga.
“Ni watoto ambao hawawezi
kusaidiwa na familia ndiyo wanapokelewa katika kituo hiki cha Mt. Nicholaus na
kwa mtizamo huo, maombi hupelekwa kwa kupitia
ofisi za ustawi wa jamii kabla ya kupokelewa kituoni.” Alifafanua mama
Koster.
Wito kwa jamii, mama Koster anatoa wito kwa jamii ya watanzania kujitolea kuwahudumia watoto hao kwani kituo
hicho hupokea watu wa kujitolea “Volunteers”
kutoka nje ya nchi kama Ujerumani na wengine hutoka katika jamii ya
kitanzania walio na elimu ya malezi ya watoto.
Shukrani, Stephanie Koster mama mlezi wa kituo cha Mt.
Nicholaus anatoa shukrani zake za dhati kwa Familia ya Katibu Tawala Mkoa Kagera Bw.
Nassor Mnambira pamoja na rafiki wa familia yake kufika kituoni hapo na kutoa zawadi kwa watoto hao pia na wote
wanaoendelea kufika na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto . “Toa ulichachoa na
Bwana atakuongezea
Watoto Wenye Mtindio wa Ubongo Wakiimba na Kufurahi Mbele ya Wageni Waliowatembelea (Hawapo Pichani)
Watoto Wenye Ulemavu Pia na Wageni Waliofika Kuwaona Kituoni Kwao.
Mama Mnambira Akitoa Zawadi zake Kwa Mama Mlezi wa Kituo
Huyu ni Mmmoja wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo
Huyu ni Mmmoja wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo
Mtoto Huyu Ana Tatizo la Ugonjwa
Ngozi Lakini Kabla ya Kuletwa Kituoni Wazazi wake na Jamii Ilimtenga kwa
Kumjengea Kijumba Chake Mwenyewe na Aliishi Peke Yake, Lakini Sasa
Anajumuika na Watoto Wenziwe.
Mke wa Katibu Tawala Mkoa Kagera Mama Mnambira Akionyesha Upendo Kwa Mtoto Huyu Kwa Kumgongea na Kinywaji Chake.
Pia Ujumbe Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Ulikuwepo Katika Kutoa Chochote kwa Watoto hao wahitaji
Picha ya Baada ya Kufurahia
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment