AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU
Wanafunzi wake wakamwuliza Wakisema Radi, ni yupi aliyetenda
dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata zaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu
hakutenda dhambi wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.
Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana na usiku
waja asipoweza mtu kufanya kazi. Muda nilipo ulimwenguni mimi ni nuru ya
ulimwengu. Alipokwisha kusema hayo alitema mate chini, akaifanya tope kwa yale
mate. Akampaka kipofu tope za macho, akamwambia Nenda kanawe katika birika ya
Siloamu, basi akaenda na kunawa; akarudi anaona. Basi jirani zake na wale
waliomwona zamani kuwa ni mwombaji wakasema, Je! Huyu si Yule aliyekuwa akiketi
na kuomba? Wengine wakasema, ndiye wengine wakasema La, lakini amefanana naye.
Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye.
Mwandishi wa kitabu hiki
amenikumbusha mbali, hasa kutokana na mitazamo hasi katika jamii dhidi ya
walemavu kwa ujumla, ila pia nimepata amani hasa nilipotazama kumbe mitazamo
hasi dhidi ya walemavu haikuanza jana wala leo ni suala lenye muda mrefu sana
katika ulimwengu huu, hata yesu pia alikutana na maswali kutoka kwa wanafunzi
wake kuhusu watu wenye ulemavu ila jambo kubwa Yesu alilolifanya ni kuoneshwa
ukuu wa Mungu kwa kumponya mtu Yule.
Kwa upande wa jamii yangu na
taifa langu kwa ujumla kwa kuwa hatuna uwezo wa kuwaponya watu enye ulemavu ila
nasi bado tuna nafasi ya kufanya jambo zuri kama Yesu alivyofanya, sisi nafsi
tuliyonayo ni kuachana na mitazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu,
tuwachukulie kama watu wengine wasio na ulemavu, kikubwa tutambue kama ilivyo
ufupi, urefu, unene, wembamba, weupe, weusi vyote ni uumbaji wa Mungu. Ndivyo
ilivyo kwa ulemavu, mtu mwenye ulemavu na asiye na ulemavu wote ni watu wa
Mungu na wameumbwa sawa na Mungu kwa mfano wake.
TUTHAMINIANE BILA KUJALI TOFAUTI TULIZONAZO, ULEMAVU
SI MKOSI WALA LAANA ILA YOTE NI KAZI YA
MUNGU, NA SIKU ZOTE KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA.
Comments
Post a Comment