WATOTO WALEMAVU WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA HUDUMA ZAO SHULENI
Na Fabiola Nassib wa HEAR MY VOICE-Arusha Watoto wenye walemavu waishio mkoani Arusha wameililia serikali juu ya kuboresha mfumo wa elimu hasa sekondari unaowatenga hali inayowafanya kukata tamaa ya kuthamini elimu. Wakiongea na HEAR MY VOICE ilipotembelea shule ya msingi Meru kwa niaba ya wanafunzi wenzake wenye ulemavu wa aina tofauti tofauti Brenda Honest mwenye ulemavu wa kutosikia (KIZIWI) alisema kuwa mfumo wa elimu hasa wa shule za sekondari hau wajali wala kuthamini walemavu kama wao. Brenda aliendelea kusema kusema kuwa ingawa wao ni walemavu lakini jamii itambue kuwa ulemavu huo hawakuuchagua hivyo ameiomba serikali na jamii yote kwa ujumla kuwasaidia kwa kuwasapoti katika mambo mbali mbali zitakazowawezesha kujitegemea hapo baadae na siyo kuwa tegemezi siku zote za maisha yao. Akitolea mfano mambo wanayohitaji kuungwa mkono Brenda alisema kuwa mfumo wa elimu hasa katika shule za sekondari na kuendelea, haijawapa kipaumbele walemavu hasa w...