MUNGU NDIYE MUUMBA NA ATAKAVYO PANGA HAKUNA ANAYEWEZA KUPANGUA. YOTE NI MAPENZI YAKE.!!!
Watoto mapacha wa kiume wamezaliwa huko India wakiwa na vichwa viwili katika mwili mmoja kitu ambacho inasemekana ni nadra sana kutokea.
Kwa mujibu wa taarifa ya Daily Mail, nervous system ya watoto hao imetengana wakati uti wa mgongo umeungana na pia wanashare sehemu ya ubavu.
Dr. S.D. Sharma, wa J.K. Lone Hospital amesema tatizo kama hilo ni nadra sana kutokea hususan kwa watoto wa kiume, na linafahamika kama ‘Dicephalic Parapagus’. Aliongeza kuwa tukio hilo ni la pili kutokea India.
Daktari huyo aliendelea kusema kuwa mara nyingi watoto wenye ‘Dicephalic Parapagus’ huzaliwa wakiwa wamekufa, na mara nyingi hutokea kwa watoto wa kike. Kwa mujibu wa Sharma alisema kuna uwezekano wa kuokoa maisha ya mapacha hao.
Tatizo
kama hilo lililowahi kutokea kwa mapacha wa kike kutoka Sudan mwaka
(2011) ambao waliozaliwa wakiwa wameungana vichwa. Watoto hao Rital na
Ritag Gaboura walifanikiwa kutenganishwa salama japo kwa tatizo kama lao
uwezekano wa kupona hua ni kwa mmoja kati ya million kumi
Rital na Ritag Gaboura wa Sudan baada ya kutenganishwa
Inasemekana tatizo la mapacha kuzaliwa wameungana hutokea mara moja kati ya watoto 100,000 wanaozaliwa.
MUNGU WEWE NI MWANIFU, SI MKOSI, SI LAANA WALA SI DHAMBI KUZALIWA MLEMAVU
Comments
Post a Comment