NATAMANI SIKU MOJA KUWA RAIS WA NCHI YANGU, PAMOJA NA ULEMAVU NILIONAO: MWITA CHARLES

Naitwa Mwita Charles kutoka katika wilaya ya Bunda, nina umri wa miaka 14. Nina wazazi wote wawili lakini baba anasumbuliwa na matatizo ya akili kwa sasa hivyo naishi na mama. Ninasoma shule ya msingi na niko katika  darasa la sita (6). Nina ulemavu wa viungo, nilizaliwa pasipokuwa na mikono yote miwili.


                                    MWITA AKIANDIKA KWA KUTUMIA MGUU WAKE
 Katika kusoma kwangu naandika kwa kutumia miguu. Jamii iliyo nizunguka inanichukulia kawaida, hawanitengi wala kuninyanyapaa, nacheza na kushirikiana na watoto wenzangu kama mtu wa kawaida.

Mahusiano ya mama na baba sio mazuri kwasababu wakikutana wanaanza kupigana, baba anamkaba shingo mama kwasababu ya tatizo la akili alilonalo. Mama anafanya kazi ya vibarua, anahangaika sana ili kupata pesa ya kunitunza na kunisomesha.Maendeleo yangu darasani ni mazuri sana kwakweli. Natamani siku moja nije kua Rais wa nchi hii.
Naishauri serikali iwaongoze watu vizuri na kuwasaidia maskini. Pia naiomba Serikali iwatunze, kuwasomesha na kuwasaidia watu wenye ulemavu kama mimi.

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU