MAZINGIRA MAGUMU YA SHULE KWA WALEMAVU…..
MWANZONI
mwa mwaka 2009, mke wa Rais, Salma Kikwete aliitaka jamii
kutowatenga wanafunzi wenye ulemavu badala yake wasaidiwe na
kushirikishwa katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kupewa elimu
kama ilivyo kwa makundi mengine ya kijamii.
Siku
aliyotoa wito huo hakusita kusema kuwa zaidi ya Sh milioni 881 zinahitajika kwa
ajili ya kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafuzi 8700 wenye ulemavu nchini
ili waweze kujifunza katika hali mazingira mazuri.
Tunapozungumzia
mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu hatumaanishi vifaa na mahitaji
mengine ya kitaaluma pekee bali hata miundombinu kama vyumba vya
madarasa, vyoo, maktaba, maabara, mabweni na mazingira ya eneo zima la shule
Kufanya
hivi ni kuwapa fursa ya wao kujiona kuwa ni sehemu ya jamii hali itakayowapa
ari ya kujifunza sambamba na wenzao wasiokuwa na ulemavu.
Mazingira ni miongoni mwa vitu vya msingi sana
katika suala zima la elimu hasa kwa walemavu.Kuna baadhi za shule ambazo
zimejengwa na serikali kwa nia ya kutaka watoto walemavu wapelekwe shule,hata
hivyo,bado mazingira ya kujifunza katika shule nyingi hayawavutii watoto hawa
hali inayosababisha baadhi yao kukacha masomo.
Shule
nyingi hasa mijini yamelazimika kujenga majengo ya maghorofa, jambo la
kushangaza ujenzi wa majengo haya haukuzingatia mahitaji ya wanafunzi wenye
ulemavu hali inyokwanza kuingia na kutoka madarasani kama ilivyo kwa wenzo
wasio na ulemavu.
Si
majengo ya maghorofa hata zile zilizojengwa chini zikawa na wasaa wa ardhi bado
nazo hazikuwakumbuka walemavu.Zipo shule hapa nchini umbali wa kukifuata choo
kwa mfano unakaribia mita 100 au 200.Huku ni kuwatesa wanafunzi wenye ulemavu
wa miguu.
KATIKA
mizunguko yangu ya kawaida napata nafasi ya kutembelea Shule ya Uhuru
Mchanganyiko. Shule ipo maeneo ya Mtaa wa Shaurimoyo na Uhuru jijini Dar es
salaam.
Shule
hii ina mchanganyiko wa wanafunzi, wenye mahitaji maalum na wa kawaida. Catherine
Mwambe ni miongoni mwa walimu wanofundisha katika shule hii, akifundisha
wanafunzi wenye mahitaji maalumu tangu ameingia katika shule hii, Pamoja na
moyo wake wa kujitolea kufundisha watoto hao, anasema kuna changamoto nyingi
ambazo Serikali inapaswa kuzifanyia kazi kwa nguvu zote.
Catherine
anasema katika kutekeleza malengo ya Milenia, Serikali ya Tanzania ilipitisha
Sera ya Elimu kwa Wote, kwa lengo la kuhakikisha kuwa watoto wote, bila kujali
jinsia zao na tofauti zao wanapata elimu
sawa.
Catherine
anafafanua kuwa licha ya kuwepo kwa mpango huo, sera hiyo haitekelezwi
ipasavyo. “Kwa mfano, hivi sasa kuna shule nyingi za kata zinazojengwa na
selikali kwa ajili ya watoto” “Je, ni kweli Serikali imechukua hatua madhubuti
kuhakikisha kuwa majengo hayo yanajengwa kwa kuangalia hawa watoto wenye
ulemavu wanayaweza kuyamudu hasa kwa wale wenye ulemavu wa viungo”,anahoji.
Anasema
kuwa tatizo lingine kubwa ni uhaba wa walimu katika shule nyingi za walemavu, ukiangalia
kuna vyuo vingi vinavyotoa mafuzo ya ualimu nchini lakini hawaletwi katika
kufundisha katika shule zenye watoto walemavu.”Si hivyo tu pia kuna baadhi ya
wazazi bado wanawaficha watoto wenye ulemavu jambo ambalo huchangia kuwanyima
fursa mbalimbali ikiwamo kupata elimu,”anasema.
Anashauri
kwamba,ili kukabiliana na changamoto hizo, Serikali na asasi zisizo za
kiserikali zielekeze nguvu katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata elimu ya
kutosha kuhusu malezi ya watoto wenye ulemavu.”kwa kufanya hivyo
itawarahisishia walimu kuwafikia watoto wengi, pia Serikali iboreshe mazingira
ya upatikanaji wa elimu, hususan kwa watoto hao,”amesema.
MWISHO………
Comments
Post a Comment