WANAFUNZI WA SHULE YA WALEMAVU KATUMBA TWO WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA
WANAHITAJI MSAADA WA KUJENGEWA CHOO CHA KISASA KINACHOENDANA NA ULEMAVU
WAO KULIKO HIVI SASA WATOTO WANATESEKA NA KUJISAIDIA SEHEMU CHAFU NA SIO
SALAMA KWA AFYA ZAO
|
HARI YA HEWA LEO MJINI TUKUYU |
|
WANAFUNZI WA KATUMBA TWO SHULE MAALUM KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA VIUNGO, KUONA, KUSIKIA, ALBINO NA WALEMAVU WA AKILI |
|
KWA
UZALENDO WA WATU WA JAPANI KUPITIA UBAROZI WAO WAMEFADHIRI UJENZI WA
MADARASA MAWILI NA MABWENI MAWILI KATIKA SHILE YA WALEMAVU KATUMBA |
|
MABWENI MAWILI YA WATOTO WALEMAVU AMABAYO YANAJENGWA KWA HISANI YA WAJAPANI |
|
SHIDA
ILIYOPO HAPA NI UMBALI WA VYOO VILIPO NA MABWENI YA KULALA PIA MADARASA
FIKILIA MVUA ZA TUKUYU NA MTOTO ANAYE TEMBEA KWA KUTAMBAA JINSI YA
KUFIKA KUJISAIDIA NI SHIDA SANA |
|
VYOO
VILIVYOJENGWA NA SERIKALI NA KWAGHARAMA KUBWA VIMEISHIA KUBOMOKA HUKU
WATOTO WAKITAABIKA KWA KUKOSA VYOO VINAVYOENDANA NA MAHITAJI YAO |
|
HAWA
WATOTO NDIO KWANZA WANAJISAIDIA KWA KUSIMAMA MLANGONI SASA INAPOTOKEA
AMBAYE ANATEMBEA KWA KUTUMIA MIKONO NDIPO UTAONA HURUMA SANA MAANA CHOO
KINAKUWA KICHAFU MAANA HAWA WALIO NA UWEZO WA KUSIMAMA WANAJISAIDIA
HOVYO |
|
CHOO NI KICHAFU NA MIUNDOMBINU SI RAFIKI KWA WATOTO WALEMAVU |
|
WATOTO
WANAHITAJI KUSAIDIWA NA WATANZANIA WALIO NA UZALENDO NA WATANZANIA HAWA
WALIO NA MAHITAJI MAALUM U ILI WAFIKIE NDOTO ZA KUPATA ELIMU KAMA
WENGINE |
|
JAMANI MIUNDO MBINU YA HAPA SIO RAFIKI KWA WATOTO WETU |
|
HIKI CHOO NI KIMEJENGWA TANGU MWAKA 2008 TANGU KIPINDI HICHO KIMEFIKIA HAPO |
|
NAKUMBUKA MWAKA 2008 NIKIWA NIMETOKEA CHUONI NIKAHAMASISHWA NA NDUGU
YANGU MICHAEL MHAGAMA KUPITIA KAMPUNI YAKE YA UJENZI ILI TUSHIRIKI
PAMOJA UJENZI WA CHOO JAPO ANGALAU KIWE RAFIKI KWA WATOTO WALIO NA
ULEMAVU KATIKA SHULE HII YA KATUMBA TWO.
NAKUMBUKA KILA MFANYAKAZI WA KAMPUNI ALIKUWA ANACHANGIA TSH 10,000/= NA
KWA KIPINDI KILE TULIFANIKIWA KUJENGA CHOO CHENYE MATUNDU SITA NA
MATANKI YAKE PAMOJA NA MASINKI YAKE LAKINI BAADA YA UJENZI HUO MAMBO
HAYAKUKAMILIKA ILI WATOTO WAANZE KUKUTUMIA CHOO.
KWAHIYO TANGU MWAKA HUO CHOO BADO HAKIJAKAMILIKA HASA MIUNDOMBINU YA
MAJI NA KUPELEKEA CHOO HIKI KUTOTUMIKA. SASA IMENIBIDI NIFIKE TENA HAPA
SHULENI KUJUA NINI KIMEBAKI ILI CHOO KIWETAYARI NA WATOTO WAENDELEE
KUTUMIA KULIKO SASA WATOTO WETU HAWANA CHOO KINACHOENDANA NA ULEMAVU WAO
OMBI LANGU NI WADAU WA HUU MTANDAO KWA WALE WALIO NA MAPENZI MEMA KWA
WATOTO WETU KUJITOKEZA ILI WATOTO WETU TUWAMALIZIE UJENZI WA CHOO PAMOJA
NA MIUNDO MBINU YA KOLIDO LA KWENDEA CHOONI ILI KUJIKINGA NA MVUA,
KULIKO WANAVYOTUMIA VYOO AMBAVYO VINASABABISHA WATOTO KUPATA MAGONJWA AU
WANAPOISHIA KUJISAIDIA VICHAKANI
NIMEONGEA NA MKUU WA SHULE HII YA KATUMBA TWO ILI KUJUA GHARAMA ZA
UJENZI ULIOBAKIA ILI KUJIPANGA KUMALIZIA CHOO HICHO AU KUJENGA KINGINE
HIVYO AMENIAHIDI KUWA ATAMTAFUTA MTAALAM ILI TUJUE THAMANI YA VITU
VILIVYOSALIA KUMALIZIA UJENZI WA CHOO HIKI.
|
MWL
OMWILE KALYOTO MWALIMU MKUU WA SHULE MAALUMU YA WALEMAVU. MWALIMU
KALYOTO AMESEMA KUWA WATOTO WALIOPO HAPO NI WALEMAVU WA VIUNGO, WALEMAVU
WA KUSIKIA, WALEMAVU WA KUONA, WALEMAVU WA AKILI PIA NA WALEMAVU WA
NGOZI YAANI ALBINO. |
|
WATOTO WAKO MICHEZONI WAKATI WA MAPUMZIKO |
|
MAZINGIRA DUNI YA KUJISOMEA KWA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUONA NA VIFAA DUNI HADI KUFIKIA KUTUMIA MAWE ILI KUJIFUNZA KUHESABU |
|
KALAKANA YA KUTENGENEZEA VIATU VYA WATOTO WALIO NA ULEMAVU MBALIMBALI WA VIUNGO |
|
WATOTO
ZAIDI YA MIA MOJA AMBAO WANASHIDA YA KUONA WANAUHITAJI WA MASHINE HII
YA KUANDIKIA LAKINI HAPO SHULENI PANA MASHINE TANO TU KITU KINACHOWAPA
SHIDA SANA KUJIFUNZA. KWA WALIO NA MAPENZI MEMA HII MASHINE INAITWA
BREILA NA DUKANI INAUZWA MILIONI MBILITU |
|
PIA
KUNA VIFAA MAALUM VYA KUHESABIA NA KALATTASI MAALUM ZA KUANDIKIA HAPA
SHULENI NI SHIDA SANA KWA KUWA SHULE INAPATA BAJETI NDOGO SANA KUTOKA
TAMISEMI AMBAYO HAIKIDHI MAHITAJI YA WATOTO SHULENI HAPO |
|
SEHEM WANAPO LALA WATOTO |
|
NIKAPATA
NAFASI YA KUZUNGUMZA JAPAO NA WANAFUNZI WACHACHE KULICHONIFURAHISHA
WATOTO HAWA NI KUTAMBUA KUWA SERIKALI INAWATHAMINI SANA KWA KUWA
SERIKALI INAWAPA NAULI NA WALIMU WA KUWACHUKUA MAJUMBANI NA KUWARUDISHA
SHULENI HAPO, PIA CHAKULA CHAO NI KIZURI NA ZAIDI WAKASHUKURU SANA WADAU
WA SHULE HIYO WANAJITOKEZA KUWAHUDUMIA KWA MAVAZI , CHAKULA NA SASA
WAFADHIRI WA KIJAPANI WANAOENDELEA NA UJENZI WA MADARASA MATATU NA
UJENZI WA MABWENI MAWILI |
|
SASA
UKAFIKA WAKATI WA KILA MTU ANATOA MACHOZI MAANA WATOTO WALIO WENGI
WAZAZI WAO NI KAMA WAMEWATELEKEZA KABISA HATA SALAMU WALA KUWATEMBELEA
HIVYO WANAKABIRIANA NA MAISHA MAGUMU SANA KWA KUKOSA MAHITAJI YA MUHIMU
KAMA MAVAZI, SABUNI, SALE ZA SHULE, VIATU NA HATA VIFAA VYA MADARASANI.
HIVYO WAMEWATAKA WAZAZI WASIWATELEKEZE KIASI HICHO KWAKUWA WAO WANA
NDOTO ZA MAISHA KAMA WALIVYO WATOTO WATOTO WASIO NA ULEMAVU. |
NAYE MWALIMU MKUU AMETHIBITISHA HILI KUWA WAZAZI WALIOWENGI HAWATAKI
KUWAHUDUMIA WATOTO WAO WAKIWA SHULENI HIVYO WATOTO HUKOSA MAHITAJI YA
MUHIMU HIVYO MAISHA YA SHULENI HAPO HUWA MAGUMU JAPO SERIKALI
HUWAHUDUMIA WATOTO HAWA KWA KIASI KIKUBWA
WADAU NAKARIBISHA MAWAZO NIJINSI GANI TUPATE SURUHISHO LA WATOTO WETU
ILI WAPATE CHOO CHA KISASA MAANA WAJAPANI WAMETUSAIDIA KUJENGA MADARASA
MATATU NA MABWENI MAWILI NAMI NAJUA KWA HILI LA CHOO TUTALIWEZA.
KARIBUNI KWA MICHANGO YA MAWAZO NA MALI PIA.
SOURCE
kingotanzania
0752881456 & 0716989978
allykingo@yahoo.com
...................................
Comments
Post a Comment