ULEMAVU WA MTOTO OINI SI MKOSI WALA LAANA....
Mtoto mwenye ulemavu, Oini Meng’ariki akiwa nyumbani baada ya kutoka
shuleni katika Kijiji cha Kivululu wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha. Picha
na Filbert Rweyemamu
Hata vidole vyake haviko sawa vilivyo vidole vya miguu vya watu walio
wengi. Kwa ujumla ana tofauti ya namna miguu yake ilivyo ukilinganisha
na watu walio wengi.
Oini Meng’oriki ni mtoto aliyezaliwa Septemba 11,2009; ni miongoni mwa
watoto waliozaliwa akiwa na ulemavu wa viungo, hana mikono na miguu yake
ina ulemavu kiasi kwamba hawezi kutembea.
Ni kwamba miguu yake imepinda, kiasi kwamba hata kukanyaga chini ili atembee inakuwa ngumu.
Hata vidole vyake haviko sawa vilivyo vidole vya miguu vya watu walio
wengi. Kwa ujumla ana tofauti ya namna miguu yake ilivyo ukilinganisha
na watu walio wengi.
Hata hivyo ukionana nae utatamani kuendelea kuwa nae kutokana na
kuonekana mwenye tabia njema, sura ya matumaini na kuonyesha furaha muda
mwingi wa maisha yake.
Tabia yake ya furaha, imesabisha awe na marafiki wengi, licha ya udogo wake wa umri.
Oini ni mtoto wa kwanza kwa mama yake Eva Meng’oriki (21) akiwa ni mke
wa tatu kwa mume wake Meng’oriki Sumeno mkazi wa Kijiji cha Kambala,Wami
Dakawa Wilaya ya Mvomero, Morogoro katika jamii ya wafugaji wa Kimasai.
Eva anasema baada ya kujifungua na kuona mtoto aliyempata ana ulemavu alishtuka kwa vile hajawahi kutokewa.
“Kama mwanadamu mwingine yeyote nilishtuka, lakini baada niliona haya ni
mambo ya kawaida, naamini ni mpango wa Mungu, hakuna la kufanya zaidi
ya kumpenda na kuahidi kumtunza,” anasema.
Anaongeza kuwa “Naamini Mungu ni kila kitu katika maisha yetu yeye akiamua kitu fulani hakuna wa kukipinga,” anasema.
Anaongeza kuwa “Nisingeweza kumkufuru Mungu wala kumlaumu kwa lolote,
kwani amenipatia mtoto ambaye ana ulemavu kwa mapenzi yake na anajua
kwanini imekuwa hivi.
“Jambo la kushangaza ni kwamba baadhi ya wanawake niliokuwa nao
hospitali ya Bwagala,Turiani baada ya kujifungua waliniambia
nisimnyonyeshe ili afe kwa njaa.
“Nilisononeka sana kuambiwa kauli ile, nilichojifunza ni kwamba huenda
kuna walemavu wengi wanauawa, kwani ni wanawake wengi waliokuwa
wakinishauri nimuue, namshukuru Mungu kwamba sikuwahi kukubaliana na
ushauri wao hata kidogo, sikutaka mwanangu afe, niliona kama ni
mashetani wale waliokuwa wakinishauri huo unyama.
Comments
Post a Comment