MAZINGIRA YA VYOO VYA SHULE MTIHANI KWA WALEMAVU
Unapozungumzia mazingira mazuri kwa
wanafunzi wenye ulemavu hatumaanishi vifaa na mahitaji mengine ya kitaaluma
pekee bali hata miundombinu kama vyumba vya madarasa, vyoo, maktaba,
maabara, mabweni na mazingira ya eneo zima la shule
Kufanya hivi ni kuwapa fursa ya wao
kujiona kuwa ni sehemu ya jamii hali itakayowapa ari ya kujifunza sambamba na
wenzao wasiokuwa na ulemavu.
Hata hivyo, uchunguzi wangu mdogo
umebaini kuwa pamoja na nia ya serikali kutaka watoto walemavu wapelekwe shule
bado mazingira ya kujifunza katika shule nyingi hayawavutii watoto hawa hali
inayosababisha baadhi yao kukacha masomo.
Hivi leo serikali kupitia mipango
kama MMEM, MMES na ujenzi wa shule za kata imefanikiwa kujenga shule nyingi kwa
lengo la kutoa fursa zaidi kwa vijana wa Tanzania wanaopata elimu katika
madaraja mbalimbali. Lakini ujenzi wa shule hizi umekuwa kikwazo kwa baadhi ya
watoto kwa kuwa hali zao za kimaumbile zinawapa ugumu kurandana na hali ya
mazingira ya shule.
Peter Nelson anasoma katika
shule Uhuru mchanganyiko alisema kuwa,
“ Shule ya uhuru mchanganyiko amesema mbali na majengo
kujengwa magorofa lakini tatizo kubwa hasa ni vyoo,hivyo maisha yanatuwia
vigumu kwa sisi walemavu maana tunashindwa kupanda maghorofa na vyoo pia vibovu
sana tunakanyaga uchafu wakati wa kwenda kujisaidia ”
Amesema shule nyingi zinazojengwa na
serikali bado hawaangalii hali yetu kwa mazingira ya vyoo, inasababisha sisi
kuugua mara kwa mara.
Zenah Juma pia ni mwanafunzi wa
shule hiyo alikuwa na haya ya kusema
“Ni kweli kama alivyosema mwenzangu ujenzi wa vyoo ni tatizo
kubwa sana kwetu kwasababu linasababisha tupate maradhi kaka
kichocho,kipundupindu hasa kwa sisi walemavu wa miguu tunaotumia mikono
kutembelea”.
Kwahiyo serikali inatakiwa kuwa
makini na suala zima la ujenzi wa shule unaoendelea kuangalia na walemavu
wanapaswa kujengewa vyoo vya kukidhi haja zao, maana hali hiyo ikiendelea
walemavu watapata magonjwa mengi na kushindwa kuhudhuria masomo yao.
Comments
Post a Comment