MKUU WA MKOA WA RUKWA AMTEMBELEA MAMA MARIANNE MJERUMANI ALIYEHAMIA TANZANIA NA KUJITOLEA KULEA WATOTO YATIMA 12.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa 
Injinia Stella Manyanya akiteta jambo na Mama Marianne Lwanetzki  raia 
wa Ujerumani alipomtembelea nyumbani kwake jana kujionea maisha ya mama 
huyo ambae kwa sasa anaishi Mkoani Rukwa katika nyumba yake inayoitwa 
'Kinder House" na watoto yatima 12 ambao aliamua kuwachukua kutoka 
katika mazingira magumu na kuishi nao kama watoto wake huku akiwapatia 
huduma mbalimbali za chakula, malazi, elimu na tiba. Watoto hao yatima 
wapo wanaume sita na wanawake ni sita.

Mtoto
 Kastory Mabruki ambaye ametajwa kuwa na sifa mbalimbali ikiwemo 
Uongozaji wa kwaya kama inavyoonekana pichani na hata uongozaji wa 
midahalo"debate" mbalimbali shuleni kwao zikiwemo za wanafunzi wa 
madarasa ya juu zaidi ya lile analosoma na kuzimudu vizuri. Katika 
watoto hao 12 kila mmoja anaonekana kuwa na kipaji cha aina yake ambapo 
Mama yao Mlezi anajitahidi kuviendeleza na kuvipa nafasi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa 
Injinia Stella Manyanya akiongea kumpongeza Mama Marianne kwa juhudi 
alizozichukua ambapo ameguswa sana na mpango huo wa mtu binafsi kulea 
watoto kama familia moja tofauti na sehemu nyingine nyingi 
ambazo taasisi ndizo zinazojishughulisha na vituo vya kulelea mayatima. 
Mkuu huyo wa Mkoa amewaasa watanzania wenye uwezo kuiga mfano huo 
kusaidia jamii kuondokana na kero za watoto wa mitaani.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa 
Injinia Stella Manyanya (katikati mbele waliokaa) akiwa kwenye picha ya 
pamoja na Mama Marianne Lwanetzki (wapili kushoto mbele waliokaa) raia 
wa Ujerumani na watoto yatima 12 alioamua kuwachukua na kuwalea kama 
watoto wake wakitokea katika mazingira magumu na ambao anaishi nao 
katika nyumba yake anayoiita "Kinder House" iliyopo katika Manispaa ya 
Sumbawanga Mkoani Rukwa. Mama huyo anawapatia watoto hao mahitaji yao 
yote ikiwemo chakula, malazi na elimu. Kulia ni Katibu wa Mhe. Manyanya 
Frank Mateni.  
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa 
Injinia Stella Manyanya (watatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na
 Mama Marianne Lwanetzki (watatu kulia) raia wa Ujerumani na watoto 
yatima 12 alioamua kuwachukua na kuwalea kama watoto wake wakitokea 
katika mazingira magumu na ambao anaishi nao katika nyumba yake 
anayoiita "Kinder House" iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani 
Rukwa. Mama huyo anawapatia watoto hao mahitaji yao yote ikiwemo 
chakula, malazi na elimu. Wapili kulia ni Hamza Temba - Afisa Habari 
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.

Nyumba hii inajulikana 
kama "KINDER HOUSE" ambapo kwa mujibu wa Mama mwenye nyumba hii Marianne
 Lwanetzki ambae ni raia wa Ujerumani alisema neno "kinder" kijerumani 
lina maana ya watoto. Mama Marianne amesema nyumba hiyo ambayo ni kubwa 
ikiwa na eneo la kutosha ameshaiandikia kisheria na kwamba ni urithi kwa
 watoto hao 12 anaowalea hata kama hatokuwepo tena duniani basi hapo 
ndipo nyumbani kwao.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa 
akiagana na familia ya Mama Marianne Lwanetzki yenye watoto yatima 12 
pamoja na wafanyakazi wake wanaomsaidia kwenye shughuli za malezi. (Na 
Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
Katika historia yake fupi Mama huyo 
alifika Mkoani Rukwa kwa shughuli za kitalii na ndipo alipomuona mtoto 
mmoja katika moja ya kituo cha kulelea mayatima akiwa na hali mbaya ya 
kiafya huku akiwa mgojwa sana, Aliamua kumchukua mtoto huyo na kuishi 
nae hadi akapona ndipo aliposhawishika na kuamua kuhamia Tanzania na 
kuchukua watoto wengine yatima hadi kufikia 12 ambao kwasasa amesema 
wanatosha kulingana na uwezo alionao.
Aliongeza kuwa katika kuwalea watoto hao anatumia uwezo wake yeye binafsi pamoja na misaada mbalimbali kutoa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa nchini kwake Ujerumani.
Aliongeza kuwa katika kuwalea watoto hao anatumia uwezo wake yeye binafsi pamoja na misaada mbalimbali kutoa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa nchini kwake Ujerumani.
HUYU MAMA KWA KAZI YA KIPEKEE ALIYOAMUA KUIFANYA HAPA NCHINI, INAPASA AWE MFANO WA KUIGWA, KIKUBWA NILICHOJIFUNZA KWA HUYU MAMA, YEYE ANAAMINI MALI NA YOTE YA DUNIA HII NI YA KUPITA ILA JAMBO LA MAANA NA LENYE TIJA KATIKA MAISHA YA HAPA DUNIANI NI KUISHI MAISHA YANAYOMPENDEZA MUNGU HASA KWA KUISHI MAISHA AMBAYO NI YA KUWAFIKILIA PIA WENGINE, KUNA WATOTO WANAISHI MAISHA AMBAYO KILA DAKIKA WAO NI KUJUTA KWANINI WAPO KATIKA DUNIA HII, WANAMKUFURU MUNGU KWA KUWAUMBA, ILA KAMA KILA MWENYE UWEZO ANGEYATAZAMA HAYA MAISHA KAMA HUYU MAMA, NAAMINI WATOTO WA MITAANI, YATIMA NA WENGINE WOTE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI WANGEIONA HII DUNIA NI SEHEMU NZURI YA KUISHI. 
Comments
Post a Comment