Popular posts from this blog
WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA
Ukatili dhidi ya watoto umeongeza idadi ya watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi licha ya kuwepo juhudi za kupambana na tatizo hilo. Watoto wanaoishi katika mazingira hayo, huathirika kisaikolojia kutokana na kujiingiza katika vitendo vya matumizi ya gundi na dawa za kulevya, huku sehemu ya jamii katika ngazi ya familia na kuficha tatizo badala ya kulipeleka kwenye vyombo vya dola. Wanafanya hivyo kwa maelezo kuwa wanaogopa aibu, matokeo yake kuna ongezeko la watoto wa mtaani, baadhi ambao bado wapo chini ya matunzo ya wazazi wao, lakini wanajiingiza katika tabia ya kuomba fedha na wanaonekana mitaani katika miji mbali mbali nchini. Ukatili unafanyika dhidi ya watoto kuanzia ngazi ya familia na ndugu wa karibu kwa kumbaka au kumlawiti mtoto anyeishi nao. Sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009, inalenga kurekebisha na kuimarisha sheria zote zihusuzo watoto, kuainisha haki, kukuza na kulinda maslahi bora ya watoto kwa mujibu wa sh...
AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU
YOHANA 9:2-7 Wanafunzi wake wakamwuliza Wakisema Radi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata zaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana na usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. Muda nilipo ulimwenguni mimi ni nuru ya ulimwengu. Alipokwisha kusema hayo alitema mate chini, akaifanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, akamwambia Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, basi akaenda na kunawa; akarudi anaona. Basi jirani zake na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji wakasema, Je! Huyu si Yule aliyekuwa akiketi na kuomba? Wengine wakasema, ndiye wengine wakasema La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. Mwandishi wa kitabu hiki amenikumbusha mbali, hasa kutokana na mitazamo hasi katika jamii dhidi ya walemavu kwa ujumla, ila pia nimepata amani hasa nili...
TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU
Stephanie Koster Mama Mlezi wa Kituo cha Mt. Nicholaus Children Center Akisoma Historia ya Kituo Kwa Wageni Waliotembelea Kituo hapo tarehe 05/02/2013 Mwanadamu mkamilifu apoamka asubuhi na kuanza siku yake kwa kutekeleza majukumu yake ya kawaida ya kila siku ya kujiingizia kipato halali cha kujikimu na kuyafanya maisha yasonge mbele huwa siyo rahisi kukumbuka kuwa kuna binadamu ambao wanahitaji msaada na uangalizi wa karibu sana. Mashirika, Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi aidha watu mmoja mmoja katika kuangalia makundi maalum ya kusaidia mara nyingi huwakumbuka watoto yatima na waishio katika mazingira magumu, wazee na walemavu wa viungo. Lakini kuna kundi maalum ambalo jamii hulisahau bila kulipa kipaumbele.. Walemavu wenye utindio wa ubongo katika jamii zetu za kitanzania husaulika sana na kuachwa bila msaada wowote wa karibu, mfano kupatiwa huduma ya karibu kama huduma za kiafya, elimu aidha kuwa na mahusiano ya kawaida...
Comments
Post a Comment