HUU NI UNYAMA KWA WATOTO
Moja kati ya ajira mbaya kwa watoto mkoani Iringa, huu mzigo ni mzito sana.
Mtoto anatumikishwa kama myama
Watoto wakazi wa Wangama wilaya ya Njombe mkoani Iringa ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja wakikokota mkokoteni wa kuvutwa na wanyama ,wakielekea kubeba mahindi shambani kama walivyokutwa leo majira ya jioni, kwa kawaida mkokoteni huu hukokotwa na Ng'ombe au Punda ila kutokana na ugumu wa maisha watoto hawa wanajiingiza katika kazi ya namna hii.
WITO KWA WANANCHI WOTE.
Hata kama hatuwezi kuwasaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu bila kuwafanyisha kazi, ni vizuri tukaangalia hata kazi za kuwapa, hivi kweli huu ni ubinadamu kumpatia mtoto kazi zinazotakiwa kufanywa na gari au wanyama? HEAR MY VOICE inatoa wito kwa wanajamii kuwa na moyo wa huruma na hawa watoto kwani hawakupenda kuzaliwa katika hali waliyonayo.
Comments
Post a Comment