UNICEF: KUTOWATENGA WATOTO WALEMAVU KUNAFAIDISHA JAMII NZIMA
   Kujumuisha watoto walio na ulemavu kuna faidi katika jamii,UNICEF  Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema  watoto wengi na vijana wenye ulemavu bado hukumbana na aina nyingi za  ubaguzi na kutengwa, na hivyo kunyimwa fursa ya kuishi kikamilifu na  kuchangia maendeleo ya kijamii, kitamaduni na kiuchumi mahali  wanakoishi. George Njogopa na taarifa kamili.  (TAARIFA YA GEORGE)  Katika taarifa yake ya kila mwaka juu ya hali ya ustawi wa watoto  UNICEF imesema kuwa watoto wanakabiliwa na hali ya ulemavu wanakabiliwa  na mazingira magumu ya kufikiwa na hudumu muhimu ikiwemo matibabu na  fursa ya kwenda shule.  Ama ripoti hiyo imebainisha kuwa watoto hao wanaandamwa na jinamizi  jinginekamavile kukumbwa na vitendo vya unyanyasaji,mateso,kupuuzwa na  kuachwa katika mazingira hatarishi.  Ripoti hiyo imesema kuwa watoto wenye ulemavu hawapaswi  kutizamwakamachombo kinachosubiriwa kupatiwa hisani ya misaada, bali ni  watoto wenye haki zote ikiwemo haki ya ku...
 
