TATIZO SUGU
MAZINGIRA MAGUMU YA KUJIFUNZIA NI CHANZO CHA UTORO KWA WANAFUNZI WENYE WALEMAVU WILAYANI NAMTUMBO. Wanafunzi walemavu wa akili shule ya msingi Namtumbo wakiwa ofisi ya walimu.Wanafunzi hawa hawana darasa maalumu la kusomea kwani wakati mwingine huchuliwa na mwalimu wao na kuwapeleka nyumbani kwake ili kuwapatia chai na kuwafundishia nyumbani kwake. Ukosefu wa chakula na madarasa ya kusomea kwa wanafunzi walemavu umesababisha wanafunzi hawa kuwa na mahudhurio madogo na wengine kutokuhudhuria kabisa. Mwalimu wa kitengo maalumu cha shule ya msingi Namtumbo Bw Lezile Kampango amesema changamoto kubwa katika kituo hicho pekee cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili wilayani namtumbo ni ukosefu wa chakula,vifaa vya kufundishia, madarasa na walimu. “Watoto kama hawa hawawezi kusoma bila chakula, kwani mwanafunzi akihisi njaa tu anatoka nje na kurudi kwao bila hata ya kuuliza, gari ikipita wote wanatoka na k