SHERIA YA MTOTO
HAKI
ZA WATOTO WALEMAVU 
Mtoto mwenye ulemavu
anastahili kupata huduma maalumu ya matibabu na nafasi sawa ya elimu na mazoezi
pale inapowezekana ili kumsaidia kufikia malengo yake ya maisha. 
Mtoto ana haki ya kutumia
kwa busara mali ya mzazi wake aliyefariki. Hakuna mtu atakayemzuia mtoto mwenye
ulemavu kutumia kwa busara mali ya mzazi wake alyefariki. 
WAJIBU WA MZAZI 
Chini ya Sheria ya Mtoto
mzazi, mlezi, ndugu au mtu au taasisi yeyote inayomlea mtoto mwenye ulemavu  ina wajibu wa kumtunza. 
Wajibu wa Mzazi au Mlezi Kutunza Mtoto 
Ni wajibu wa mzazi, mlezi au
mtu yeyote anayekaa na mtoto mwenye ulemavu kumtunza   kwa
kumpatia haki na mahitaji yafuatayo;- 
a)
Chakula; 
b)
Makazi; 
c)
Mavazi; 
d)
Matibabu ikiwa ni pamoja na kupata chanjo; 
e)
Elimu na malezi; 
f)
Uhuru; na 
g) Haki ya kucheza na
kupumzika 
Vilevile mtu yeyote
haruhusiwi kwa makusudi kumzuia mtoto mwenye ulemavu kupata elimu, chanjo,
chakula, makazi, matibabu ya kiafya, au kumnyima mtoto mwenye ulemavu kitu
chochote kinachohitajika katika maendeleo na ustawi wake. 
Comments
Post a Comment