ANGALIZO KWA JAMII.
AJIRA KWA WATOTO
Mtoto
mwenye umri wa kuanzia miaka 14 ana haki ya kufanya kazi nyepesi na kupata
malipo stahiki.
Angalizo
Ieleweke
kuwa, kazi nyepesi ni zile ambazo haziathiri afya ya mtoto, hazikwamishi
maendeleo yake kielimu au makuzi yake. Hii ni pamoja na kazi ambazo hazina
madhara katika utendaji wa kazi za kimasomo zinazotolewa ili azifanye akiwa
nyumbani, haki yake ya kucheza, au kazi ambazo haziathiri uhuru wake wa
kushiriki katika mafunzo ya kijamii.
Kwa
hali hiyo, mtu haruhusiwi kumwajiri mtoto katika kazi yeyote ile ya kinyonyaji.
Pia sheria inasisitiza kuwa, mtu haruhusiwi kumwajiri mtoto katika kazi yeyote
ambayo ni hatari katika afya yake, elimu, akili, maumbile na hata katika
maendeleo yake ya kiroho.
Kazi
yeyote itahesabiwa kuwa ya kinyonyaji endapo kazi hiyo itakuwa na viashiria au
mambo yafuatayo;-
a) Inaathiri afya na makuzi ya
mtoto
b) Inazidi masaa sita kwa siku
c) Hailingani au inazidi umri
wake
d) Inamlipa mtoto malipo kidogo
na yasiyostahili; au
e)
Kazi hiyo inamhitaji mtoto kufanya kazi nyakati za usiku ambazo huanza muda
wowote kati ya saa mbili za usiku hadi saa kumi na mbili za asubuhi.
Sheria
pia inaainisha kazi hatarishi kwa mtoto kama ifuatavyo;-
a)
Zinazomfanya au kumlazimisha mtoto aingie baharini,
11
b) Zinazomfanya mtoto au
kumlazimisha mtoto aingie mgodini au kwenye machimbo ya mawe,
c) Zinazomfanya au kumlazimisha
mtoto kuponda mawe,
d) Zinazomwingiza au kumlazimisha
aingie katika viwanda ambavyo madawa huzalishwa au kutumika,
e) Zinazotumia mashine mbalimbali,
f) Kazi za baa, hoteli, na mahali
pengine popote pa starehe na,
g)
Kazi ambazo zinamweka mtoto katika mazingira ya jinsia ya mahusiano ya kingono
au ukahaba bila kujali kama analipwa au halipwi.
Hivyo
basi, kila mwajiri ambaye ameajiri watoto, anatakiwa kuhakikisha kwamba kila
mtoto aliyeajiriwa kihalali anapewa ulinzi dhidi ya mazingira yeyote ya
unyanyasaji au vitendo vyovyote vinavyoweza kumwathiri kulingana na umri wake
au uwezo wake wa kufanya kazi.
ADHABU
Mtu yeyote atakayevunja
masharti hayo anaweza fungwa kifungo cha miaka mitatu au kulipa faini
isiyopungua shilingi laki moja au vyote kwa pamoja.
Comments
Post a Comment