SIKUKUU KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU KWAO NI SIKU YA MATESO.
Baadhi ya watoto wa mitaani wakiwa wamelala nje kutokana na kukosa sehemu za kulala.Baadhi yao kwa kutaka sehemu nzuri za kulala na chakula kizuri huwa tayari kufanyiwa vitendo vibaya. Watoto kulawitiwa ili wapate hifadhi ya kulala au kupewa chakula kizuri ni sehemu ya maisha ya baadhi ya watoto waishio mitaani mjini. Hii ni siri kubwa ambayo imejificha miongoni mwao, ili uweze kupata siri hii inakulazimu lazima ujenge uhusiano wa karibu na wa muda mrefu na watoto hao. Watuhumiwa wakubwa wa kuwaingilia kinyume na maumbile watoto hao ni baadhi ya walinzi wanaolinda katika maduka ya biashara na vijana waliowazidi umri; vitendo hivyo vinaonekana kushika kasi. Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwandishi wa makala haya kwa miezi kadhaa, umebaini kuwa vitendo vichafu vimesababisha baadhi yao kuathirika kisaikolojia hivyo kujikuta wakiona jambo hilo ni la kawaida na hulifurahia. Watoto hao hufanyiwa vitendo hivyo hasa kipindi ...