SIKUKUU KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU KWAO NI SIKU YA MATESO.



Baadhi ya watoto wa mitaani wakiwa wamelala nje kutokana na kukosa sehemu za kulala.Baadhi yao kwa kutaka sehemu nzuri za kulala na chakula kizuri huwa tayari kufanyiwa vitendo vibaya. 


Watoto kulawitiwa ili wapate hifadhi ya kulala au kupewa chakula kizuri ni sehemu ya maisha ya baadhi ya watoto waishio mitaani mjini. Hii ni siri kubwa ambayo imejificha miongoni mwao, ili uweze kupata siri hii inakulazimu lazima ujenge uhusiano wa karibu na wa muda mrefu na watoto hao.
Watuhumiwa wakubwa wa kuwaingilia kinyume na maumbile watoto hao ni baadhi ya walinzi wanaolinda katika maduka ya biashara na vijana waliowazidi umri; vitendo hivyo vinaonekana  kushika kasi.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwandishi wa makala haya kwa miezi kadhaa, umebaini kuwa vitendo vichafu vimesababisha baadhi yao kuathirika kisaikolojia hivyo kujikuta wakiona jambo hilo ni la kawaida na hulifurahia.

Watoto hao hufanyiwa vitendo hivyo hasa kipindi cha masika ambapo mvua huwa zinanyesha, maeneo ambayo hupendelea kulala nyakati hizo kwenye majumba ambayo ujenzi wake haujamalizika (Mapagala) huwa yanavuja maji ya mvua hivyo hulazimika kuyakimbia kujisalimisha popote.
Wakati wa sikukuu pia kwao ni adha nyingine kutokana na baadhi ya watu wanaolewa kupita kiasi kuwabaka na kuwapiga watoto wa mitaani muda wa usiku katika maeneo mbalimbali ya mijini hasa maeneo yaliyo jirani na kumbi za starehe.
WATOTO WA MITAANI NAO WANA HAKI SAWA NA WATOTO WENGINE, BADALA YA KUWAFANYIA VITENDO VYA KIKATIRI HUU NDIO WAKATI WA KUWAONESHA UPENDO NAO WAFURAHIE SIKUKUU KAMA WATOTO WENGINE. JAMII NA SERIKALI KWA UJUMLA YATUPASA KUWATEMBELEA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU NA KUWASAIDIA KWA CHOCHOTE ILI NA WAO PIA WASHEREHEKEE SIKUKUU YA X-MASS NA MWAKA MPYA KWA FURAHA NA AMANI. PIA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU NA WALE WANAOTUMIKISHWA KATIKA AJIRA NGUMU WANAHITAJI KUSHEREHEKEA SIKUKUU KAMA WATOTO WENGINE KWA KUONESHWA UPENDO NA KUWATHAMINI.
NAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA X-MASS NA HERI YA MWAKA MPYA WENYE AMANI NA UPENDO 2014, TUZIDI KUWA MABALOZI WAZURI WA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU. PAMOJA TUTAJENGA JAMII YENYE KUTHAMINIANA BILA KUJALI TOFAUTI TULIZONAZO. 
MUNGU IBARIKI TANZANIA................... MUNGU IBARIKI HEAR MY VOICE.
IMEANDALIWA na Mwanzilishi na mmiliki wa HEAR MY VOICE BLOG SANJI MIRUMBE JAMES.(BEdSN)

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU