WATOTO WA MITAANI

Watoto wa mitaani ni watoto kama wengine na wanahaki sawa kama watoto wengine.Lakini kuna baadhi ya wanajamii wanabagua sana watoto wa mitaani na kuwapa kipaumbele sana watoto wa majumbani.
Pia wa mitaani ni moja ya makundi yanayokosa huduma muhimu kutoka kwa jamii. Watoto hao pia wapo kwenye hatari kubwa ya kutendewa vitendo viovu vya udhalilishaji na kuambukizwa virusi vya Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI).

Imekuwa kawaida katika jamii, kuwaita watoto hawa kuwa “watoto wa mitaani”, wakati mitaa haizai watoto. Watoto wengi hukimbia nyumbani kwa wazazi wao, kutokana na kukosa huduma, kunyanyaswa na wanafamilia, hasa wazazi wa kambo.

Swali la kujiuliza; kwa nini watoto hao huondoka majumbani mwao?
Watoto wengi wanaeleza sababu mbalimbali zinazofanya watoto hao kukimbilia mitaani, ambazo ni: kukataliwa na baba au mama zao wa kambo, kufiwa na wazazi na kupigwa. Wengine hutumika kama vitega uchumi vya wazazi, hasa wanaoishi mijini.

Wapo watoto wa mitaani waliofiwa na wazazi. Lakini wajomba, shangazi na ndugu wengine, hugoma kuwachukua au kuwalea watoto hao, kutokana na hali ya uchumi, ambayo husababisha wakimbilie mitaani ili kupata walau fedha za kujikimu.
Baadhi ya watoto wa mitaani hukidhi mahitaji yao wenyewe.


Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU