KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU KITAIFA IRINGA , SERIKALI YA TANZANIA YAPIGA MARUFUKU UJENZI WA MAJENGO YASIYO RAFIKI NA WALEMAVU.
  SERIKALI  imeziagiza  mamlaka  za  usafiri  wa majini na nchi kavu (SUMATRA )  nchini  kuanza mchakato  wa  kukaa na  wamiliki wa  vyombo  hivyo  ili kuanza  uangizaji  wa vyombo  vya usafiri yakiwemo mabasi ambayo ni  rafiki na walemavu nchini huku ikipiga marufuku  majengo ya   serikali kujengwa bila kuwepo kwa  mchoro  unaoonyesha mazingira yanayozingatia makundi  yote ya jamii  likiwemo la walemavu wa viungo .       Agizo   hilo  limetolewa na  waziri  mkuu Mizengo  Pinda wakati  wa maadhimisho ya  siku ya  walemavu  duniani yaliyofanyika   kitaifa  katika  viwanja  vya kichangani mkoani  Iringa jana.   Akiwahutubia   walemavu hao na  wananchi  waliofika katika  viwanja   hivyo waziri  mkuu ,aliyewakilishwa na waziri  wa nchi  ofi...
