KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU KITAIFA IRINGA , SERIKALI YA TANZANIA YAPIGA MARUFUKU UJENZI WA MAJENGO YASIYO RAFIKI NA WALEMAVU.
SERIKALI imeziagiza mamlaka za
usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA ) nchini kuanza
mchakato wa kukaa na wamiliki wa vyombo
hivyo ili kuanza uangizaji wa vyombo vya usafiri
yakiwemo mabasi ambayo ni rafiki na walemavu nchini huku ikipiga
marufuku majengo ya serikali kujengwa bila kuwepo kwa
mchoro unaoonyesha mazingira yanayozingatia makundi yote ya
jamii likiwemo la walemavu wa viungo .
Agizo hilo limetolewa na waziri
mkuu Mizengo Pinda wakati wa maadhimisho ya siku ya
walemavu duniani yaliyofanyika kitaifa katika
viwanja vya kichangani mkoani Iringa jana.
Akiwahutubia walemavu hao na wananchi
waliofika katika viwanja hivyo waziri mkuu
,aliyewakilishwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera
na uratibu wa bunge) ,Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa jimbo la
Isimani mkoani Iringa alisema kuwa kimekuwepo kilio cha
muda mwingi kutoka kwa walemavu juu ya kusaulika katika
ujenzi wa majengo mbali mbali ambayo yamekuwa
yakijengwa bila kuzingatia kundi la watu wenye
ulemavu jambo ambalo ni sawa na kuwabagua watu hao.
Hivyo alisema katika kuona kilio
hicho cha walemavu kinafanyiwa kazi kuanzia
sasa majengo yote ya serikali zikiwemo shule na taasisi
nyingine kabla ya kuanza ujenzi wake lazima
wasimamizi wa ujenzi huo kujiridhisha kwa mchoro ambao
utaonyesha mazingira yatakayomuwezesha mlemavu
kutumia jingo hilo bila usumbufu tofauti na ilivyo sasa
ambapo idadi kubwa ya majengo mazingira yake si lafiki
kwa walemavu.
" Ni siku nyingi watu wenye
ulemavu wamekuwa wakilalamika juu ya mazingira yasiyo
rafiki katika majengo mbali mbali .....sasa leo
naomba kuagiza kuwa michoro yote inayochorwa katika majengo
ya huduma za kijamii ni marufuku kupitishwa ama
wasimamizi wa ujenzi husika kuruhusu ujenzi iwapo
mchoro hauonyeshi kama utayajali makundi yote wakiwemo
walemavu.....wasimamizi wote msikubali kusimamia wala
kutangaza tenda ya ujenzi kama ramani yake si rafiki
kwa walemavu.....lakini pia hata kwenye mabasi hivi
unamtegemea mtu mwenye ulemavu wa miguu ataingia vipi na baiskeli
yake katika gari iwapo hakuna mazingira yanayomwezesha
kuingia .... hivi sasa teknlojia imezidi kukua na baadhi ya
nchi wameanza muda mrefu kuwajali walemavu kwa kuwa na mabasi ambayo
mlemavu anaingia na baiskeli yake na kushuka nayo
bila usumbufu ni vema hata Sumatra kuangalia uwezekano wa kuwajali
walemavu hao . pia ni vizuri hata nyumba za ibada nazo
ningeshauri baba askofu kuangalia kuweka mazingira "
alisema Lukuvi.
Kuhusu ombi la walemavu hao hasa
wale wasio sikia kuomba serikali kuwa na wakalimani katika
kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na vituo vingine
vya luninga ili kuwawezesha walemavu hao nao kuweza
kufuatilia hotuba ya Rais mwisho wa mwezi na mambo mengine badala
ya kutengwa ,alisema kuwa suala hilo
ni wajibu wa serikali kuwajali watu wake
hivyo tayari imeuagiza uongozi wa TBC na mamlaka ya
mawasiliano Tanzania (TCRA) kulitafutia ufumbuzi suala
hilo la mkalimani hasa katika TBC .
Katika hatua nyingine Lukuvi aliwataka
walemavu hao ili ombi lao la kutazamwa katika nafasi
za uongozi liweze kuzingatiwa ni vema wao
wenyewe kujitokeza kwa wingi kuipigia kura
katiba iliyopendekezwa pindi itakapokuja kwa wananchi kwa
madai kuwa katika katiba hiyo imezingatia mambo
mengi ya kijamii likiwemo la kuwajali watu wenye ulemavu
kwa kuwatengea nafasi nyingi zaidi na iwapo
katiba hiyo itapitishwa kazi ya msuguano wa rushwa
unaweza kuhamia kwa walemavu kwa kila mmoja kutaka kupewa
nafasi.
" Hadi hivi sasa ni chama cha mapinduzi (CCM)
pekee ambacho kina wabunge wa viti maalum wa kuteuliwa kutoka
kundi la walemavu huku vyama vingine vyote havijawakumbuka
kabisa watu wenye ulemavu ukiacha mbunge wa jimbo la
Lindi mjini pekee ambae hakupendelewa katika ubunge wake bali
alishindwa kihalali kwa kuchaguliwa na wananchi
wake..nafikiri tushirikiane kuhakikisha katiba hii
iliyopendekezwa inapita ili tuungane pamoja katika
kujenga nchi yetu "
Katika salam za walemavu waziri wa
Afya na ustawi wa jamii Dkt Seil S. Rashid zilizotolewa
kwa niaba yake na mwenyekiti wa baraza la
watu wenye ulemavu nchini na Dunford Makala alisema
kuwa wizara inaendelea kuimarisha ushirikiano na
vyama vya watu wenye ulemavu na shirikiasho la
vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA)
katika kuhakikisha utekelezaji wa uwekaji wa fursa na
haki sawa kwa watu wenye ulemavu nchini .
Alisema katika kuhakikisha ushirikiano
unakuwepo wizara yake imezindua baraza la ushauri
la Taifa la watu wenye ulemavu toka mnamo 1
Novemba 2014 na katika hilo kamwe hawataacha
kumpongeza Rais Dkt Jakaya Kikwete kwa kumteua
mwenyekiti wa baraza hilo
Aidha alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa
nchi hii chini ya Rais Dkt Kikwete imefanya mambo
mengi zaidi ya kuwajali watu wenye ulemavu
katika Nyanja za kiuchumi ,kiutamaduni na kisiasa
ambavyo vyote hivyo kumwezesha mlemavu kujikwamua
kimaisha
Hata hivyo alisema ushahidi wa
yote hayo ni pamoja na kuridhia mikataba ya kimataifa juu ya
haki za watu wenye ulemavu , kutungwa kwa sharia Na.9 ya mwaka 2010 ya
watu wenye ulemavu na kanuni zake ,kuwashirikisha watu wenye
ulemavu katika tume ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya
muungano wa Tanzania pamoja na kuteuliwa kwa wajumbe 20 wenye
ulemavu katika bunge maalumu la mabadiliko ya katiba la mwaka 2014.
Awali walemavu hao katika risala yao
iliyosomwa na makamu mwenyekiti wa SHIVYAWATA Amina
Mollel pamoja na kuishukuru serikali kwa jinsi
kwa kuendelea kuwa karibu zaidi na watu wenye
ulemavu kwa kushiriki shughuli mbali mbali za walemavu ,bado
waliweza kuishukuru serikali kwa kuandaa sera ya maendeleo ya
watu wenye ulemavu ya mwaka 2004, kutambuliwa kwa watu wenye
ulemavu katika MKUKUTA,kuwezesha kuongezeka kwa idadi ya watu wenye
ulemavu wanaopata elimu kuanzia shule za msingi hadi elimu ya juu
na mambo mengine mengi ambayo wao kama walemavu
wamekuwa wakiona serikali yao ipo pamoja nao.
Sanjari na mema hayo bado waliiomba serikali
kuzingatia kuwapatia walemavu mambo muhimu katika maisha ya kila
siku ikiwa ni pamoja na kuwa na vyombo vya usafiri rafiki kama
magari moshi.vyombo vya usafiri majini ,angani ,miundo mbinu katika
majengo na viwanja vya ndege ambavyo vitamwezesha
mlemavu pia kuwa huru .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema
kuwa maadhimisho hayo yaliyofanyika chini ya kauli mbiu
isemayo " Maendeleo endelevu ;Ahadi ya Teknolojia huku
mkoa wa Iringa ukiendelea kuwa bega kwa
bega na walemavu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi karibu
na vyama hivyo vya watu wenye
ulemavu na kuwa mkoa huo kwa sasa una jumla ya
walemavu zaidi ya 179 ,000 na wote serikali
imeendelea kuwalinda na kuwa nao pamoja.
Comments
Post a Comment