Muone MTU si ULEMAVU ALIONAO.

see the person not the disability

MUONE MTU NA SI ULEMAVU WAKE, Ni maneno machache sana ila yana maana kubwa sana miongoni mwetu, siku zote tunauona ulemavu na kujiuliza huyu mlemavu anaweza kufanya jambo gani? Binadamu wote ni sawa ulemavu ni tofauti za kimaumbile tu ila vipawa na karama Mungu alizomgawia kila mmoja zinabaki kuwa ndani ya mtu na si ndani ya ulemavu mtu alionao. 

Katika kuthibitisha kauli yangu kuna mifano mingi sana ya watu wenye ulemavu waliofanya mambo makubwa tu kuliko watu wasio walemavu, mfano watu Kama Voice wonder, Lena Maria, hawa na wengine wengi wameushangaza ulimwengu kwa sauti zao nzuri Mungu alizowajalia achilia mbali ulemavu walionao.

Ni vizuri tukamtazama mtu na si ulemavu alionao. Hiyo itatusaidia sana kuwathamini na kuwajali sana watu wenye ulemavu na hiyo itapelekea kuwapa fursa sawa na watu wasio na ulemavu.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU