UJUMBE WA SIKU YA WALEMAVU DUNIANI.


 Ikiwa zimebaki takribani siku saba kabla ya kuadhimisha siku ya walemavu Duniani, kuna maswali mengi ya kujiuliza kama jamii tunayozungukwa na watoto pamoja na watu wazima wenye ulemavu wa aina tofauti tofauti, moja ya maswali hayo ni kama ifuatavyo, umeifanyia nini jamii ya watu wenye ulemavu,? umeguswa kwa namna gani na hali zao,? umekuwa ni mtu unaezidi kupotosha ukweli kuhusu ulemavu au ni mtu unayesaidia kuondoa mitazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu? Je unawasaidia walemavu kwa kuwa unawahurumia au ni kwa sababu ni jukumu lako? sambamba na maswali mengine mengi na majibu tofauti tofauti, jambo moja la msingi ni kutathimini kwa kina ukuu na uweza wa Mungu kwa kila jambo, tofauti zetu zisitufanye tukadharauliana nakutokuthaminiana.

Jambo la msingi tunapokaribia kuadhimisha siku ya walemavu Tanzania, ni kuhakikisha tunakuwa na upendo kwa watu wenye ulemavu tukiwachukulia ni sehemu muhimu ya jamii yetu, tushirikiane nao katika mambo mablimbali ya kijamii na kiuchumi kwa kujenga taifa lenye haki na usawa kwa wote bila kuangalia tofauti zetu, hiyo itatusaidia sana katika kuishi kwa amani na upendo siku zote.

Jambo la pili ni jamii nzima kuwa na mtazamo chanya dhidi ya walemavu na itakuwa rahisi pale tutakapokuwa na msimamo wa pamoja katika kuona uwezo wa mtu na si ulemavu alionao, hiyo itatufanya kuwapa nafasi watu wenye ulemavu katika mambo mbalimbali, ukweli ulio wazi ni kuwa watu wenye ulemavu bila kuwatenga na kutokuwahukumu kwa ulemavu wao wanaweza kufanya mambo makubwa ambayo hata mtu asiye na ulemavu kuna uwezekano wa kutofanya sawa na mtu mwenye ulemavu alivyofanya. Mfano mlemavu asiyeona Profesa Edward Bagandashwa pamoja na ulemavu wake amefanikiwa miongoni mwa wanazuoni nguli Tanzania na Afrika ya Mashariki hiyo yote ni kutokana na kupewa nafasi na ameweza kuitumia vizuri na kuuthibitishia ulimwengu kuwa ulemavu si kutokuweza

TUISHI KWA UPENDO NA KUTHAMINIANA WALA TOFAUTI ZETU ZISITUTENGANISHE, SISI SOTE NI MALI YA MUNGU TOFAUTI TULIZONAZO NI KATIKA KUUDHIHIRISHA UKUU WAKE KWETU.

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU