SHULE YA WALEMAVU BUHANGIJA JUMUISHI YAELEMEWA NA CHANGAMOTO
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimsikiliza kwa
makini Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija
Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi aliyekuwa akimwelezea
changamoto mbalimbali walizonazo shuleni hapo.(Picha na Zainul Mzige).
Na MOblog, Shinyanga
SHULE
ya watoto wenye ulemavu ya Buhangija Jumuishi inakabiliwa na changamoto
kubwa zinazofanya maisha kwa watoto hao kuwa magumu.
Miongoni mwa changamoto hizo ni kukosekana kwa huduma za matibabu, walimu wa kutosha na mabweni.
Hayo
yamebainika wakati wa ziara fupi ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Zulmira Rodrigues.
Mkuu
wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi
iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi, ndiye aliyeelezea ugumu
uliopo katika shule hiyo yenye wanafunzi 209 wenye ulemavu wa aina
mbalimbali.
Mkuu
wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya
mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi akimtambulisha Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefanyia ziara fupi
akiwa safarini kuelekea jijini Mwanza akiwa ameambatana na Afisa Mradi
wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias
(katikati).
Alisema
shule hiyo yenye walemavu wa aina tatu wa kusikia, ngozi na wasioona
inakabiliwa pia na lishe duni ambayo haimpi kijana nafasi ya kuendelea,
kwani wanakula mlo wa aina moja na kidogo.
Shule
hiyo ambayo awali ilikuwa inawapokea wanafunzi wasioona sasa inapokea
walemavu wa ngozi kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji
ya albino.
Aidha
mwalimu huyo alisema kwamba wameiomba serikali kuwa na muuguzi na
daktari katika makazi hayo lakini mpaka sasa hawajapatiwa kutokana na
wao wenyewe kutokuwa na uwezo wa kuwalipa.
Alisema
kutokana na rika mbalimbali na tatizo la walemavu wa ngozi shule hiyo
ambayo sasa imegeuzwa kuwa makazi inastahili kuwa na daktari na mabweni
yaongezwe.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ( wa pili kushoto)
akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani
Shinyanga (hawapo pichani) alipofanya ziara fupi akiwa safarini
kuelekea jijini Mwanza akiwa ameambatana na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya
na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias (wa pili kulia). Kulia
ni Mkuu wa kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija
Jumuishi ya mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi.
Aidha mwalimu alisema walimu kwa ajili ya viziwi hawatoshi.
Naye
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, amesema
ameyaona mazingira hayo na kuahidi kushirikiana na marafiki na mamlaka
nyingine kuboresha mazingira ya kituo hicho.
Alisema
kwamba amefurahishwa kuwapo katika kituo hicho na kuona namna
wanavyoweza kusaidia sehemu hiyo ya jamii kutojisikia upweke.
Akizungumza
na watoto hao walimwambia kwamba wana changamoto ya nguo, vitanda,
vitabu na mahitaji mengine ya lazima kama watoto na wanafunzi.
Baadhi
ya watoto wanaosoma shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani
Shinyanga wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira
Rodrigues (hayupo pichani).
Mwanafunzi
wa kidato cha pili shule ya sekondari Loreto mkoani Shinyanga Beatrice
Leme anayelelewa kwenye kituo hicho kutokana na kukithiri kwa mauaji ya
walemavu wa ngozi mkoani humo akimwelezea changamoto mbalimbali
zinazowakabili kwa niaba ya wanafunzi wenzake Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefanya ziara fupi
shuleni hapo.
Mwanafunzi
wa darasa la sita shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya mkoani
Shinyanga, Daniel Limbu akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Zulmira Rodrigues kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues, Afisa Mradi wa Elimu
ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias pamoja na Mkuu
wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi ya
mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi wakifurahi pamoja na watoto wenye
ulemavu wa ngozi katika shule hiyo.
Afisa
Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias
katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi
wanaolelewa kwenye kituo hicho ambacho ni salama kwao kutokana na hofu
iliyokuwa inalikumba taifa ya mauaji ya albino.
Baadhi
ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wakicheza mpira kwenye mazingira
salama shuleni hapo kutokana na hofu iliyokuwa inalikumba taifa ya
mauaji ya albino.
Mkuu
wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya msingi Buhangija Jumuishi
iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi akimtambulisha mtoto Erick
mwenye ulemavu wa ngozi kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania,
Zulmira Rodrigues (kushoto) aliyefanya ziara fupi kwenye kituo cha
kulelea watoto wenye ulemavu (mahitaji maalum).
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akimsuka kwenye bembea
mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi Zawadi Deus anayesoma shule ya
msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga wakati wa michezo
alipofanya ziara fupi shuleni hapo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha
wageni wakati akijiandaa kuondoka shuleni hapo baada ya kuhitimisha
ziara yake fupi. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha watoto walemavu shule ya
msingi Buhangija Jumuishi iliyopo mkoani Shinyanga Mwl. Loyce Daudi.
Comments
Post a Comment