TANZANIA: MAISHA YA HATARI YA WATOTO WACHIMBA DHAHABU
Vijana
wadogo wakike na wakiume wa Kitanzania wanashawishika kujiingiza katika
uchimbaji wa dhahabu wakitumaini kupata maisha bora, lakini baadae wanajikuta
wamekwama katika mzunguko mbaya wAa hatari na kukata tamaa. Tanzania na
wahisani wanahitaji kuwatoa watoto hawa katika migodi na kuwaingiza shuleni au
katika mafunzo ya ufundi stadi.
Janine
Morna, mtafiti wa haki za watoto wa shirika la Human Rights Watch
(Dar Es Salaam) – Watoto wenye umri mdogo wa hadi miaka
minane wanafanya kazi katika migodi midogo midogo ya dhahabu ya Tanzania, ikiwa
na hatari kubwa kwa afya zao na hata maisha yao, shirika la Human Rights Watch
imesema katika ripoti iliyotolewa leo. Serikali ya Tanzania inapaswa kukomesha
ajira kwa watoto katika uchimbaji mdogo mdogo wa dhahabu, ikiwa ni pamoja na
katika migodi isiyo rasmi, na isiyo na leseni, na Benki ya Dunia na nchi
wahisani wanapaswa kuunga mkono juhudi hizi.
Ripoti yenye kurasa 96, “Kazi ya Sulubu
yenye Sumu: Ajira kwa Watoto na Kujiweka Wazi kwa Zebaki katika Migodi Midogo
Midogo ya Dhahabu ya Tanzania,” inaelezea jinsi gani maelfu ya
watoto wanafanya kazi katika migodi midogo midogo ya dhahabu yenye leseni na
isiyo na leseni Tanzania, nchi ya nne kwa ukubwa kwa uzalishaji
wa dhahabu barani Afrika. Wanachimba na kupekesha mashimo marefu , yasiyo
imara, wakifanya kazi chini ya ardhi kwa kupeana zamu kwa hadi masaa 24, na
kusafirisha na kutwanga mifuko mizito ya mawe ya dhahabu. Watoto hawa wanakuwa
katika hatari ya kujeruhiwa kwa mashimo kuporomoka na ajari zinazoweza kutokana
na vifaa wanavyotumia, vile vile matatizo ya kiafya ya muda mrefu kutokana na
kujiweka wazi kwa zebaki, kuvuta vumbi, na kubeba mizigo mizito. Kijana mdogo
wa miaka 17 aliyenusurika katika ajali ya shimo aliiambia shirika la Human
Rights Watch, “Nilidhani nimekufa, niliogopa sana.”
“Vijana wadogo wakike na wakiume wa Kitanzania wanashawishika kujiingiza katika uchimbaji wa dhahabu wakitumaini kupata maisha bora, lakini baadae wanajikuta wamekwama katika mzunguko mbaya wa hatari na kukata tamaa,” alisema Janine Morna, mtafiti wa haki za watoto wa shirika la Human Rights Watch “Tanzania na wahisani wanahitaji kuwatoa watoto hawa katika migodi na kuwaingiza shuleni ao katika mafunzo ya ufundi stadi.”
“Vijana wadogo wakike na wakiume wa Kitanzania wanashawishika kujiingiza katika uchimbaji wa dhahabu wakitumaini kupata maisha bora, lakini baadae wanajikuta wamekwama katika mzunguko mbaya wa hatari na kukata tamaa,” alisema Janine Morna, mtafiti wa haki za watoto wa shirika la Human Rights Watch “Tanzania na wahisani wanahitaji kuwatoa watoto hawa katika migodi na kuwaingiza shuleni ao katika mafunzo ya ufundi stadi.”
Watoto wengi wanaofanya kazi za uchimbaji ni yatima au wale
wanaoishi katika mazingira hatarishi ambao hawana mahitaji ya msingi na msaada.
Shirika la Human Rights Watch iligundua pia kwamba wasichana wadogo
wanaoishi katika migodi au maeneo yanayoizunguka migodi wanakabiliwa na
unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na vishawishi vya kujiingiza katika biashara
ya ngono. Baadhi ya wasichana wanakuwa wahanga wa utumikishwaji wa biashara ya
ngono na hivyo kuwa hatarini kuambukizwa virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine
ya zinaa.
Shirika la Human Rights Watch ilitembelea migodi 11 katika
mikoa ya Geita, Shinyanga na Mbeya, na kufanya mahojiano na watu zaidi ya 200,
ikiwa ni pamoja na watoto 61 wanaofanya kazi katika machimbo madogo madogo ya
dhahabu. Ajira kwa watoto katika kazi za hatari za uchimbaji ni moja kati ya
namna mbaya kabisa za ajira kwa watoto chini ya makubaliano ya kimataifa,
ambayo Tanzania ni mwanachama ya makubaliano hayo.
“Katika makaratasi, Tanzania ina sheria madhubuti sana zinazokataza ajira kwa watoto katika uchambaji madini, lakini serikali imefanya kidogo sana katika kutekeleza sheria hizo,” alisema Morna. “Wakaguzi wa kazi wanahitaji kutembelea mara kwa mara migodi yote, ile yenye leseni na isiyo na leseni, na kuhakikisha kwamba waajiri wanapata vikwazo kwa kutumia ajira kwa watoto.”
Watumishi watoto, pamoja na wale wanaoishi maeneo ya karibu
na migodi, wapo katika athari ya kudhurika na zebaki. Zebaki hushambulia mfumo
mkuu wa fahamu na inaweza kusababisha ulemavu wa maisha kwa watoto, ambao miili
yao inayoendelea kukua inaathirika kirahisi zaidi kwa metali nzito. Wachimbaji,
pamoja na watoto, wanachanganya zebaki pamoja na mawe ya dhahabu zilizopondwa
na kuichoma aloi ya zebaki (gold-mercury amalgam) ili kuiachia dhahabu,
wakijiweka wazi kabisa na harufu kali ya moshi wa sumu wa zebaki. Hata watoto
wadogo kabisa ambao hawafanyi kazi huwa wanakuwepo wakati wa zoezi hili, ambalo
nyakati zingine hufanywa nyumbani.
Watu wazima wengi na wachimbaji watoto hawafahamu hatari
hizi za kiafya. Wahudumu wa afya hawana mafunzo na hawana vifaa vya kutibia na
wanakosa zana za uchunguzi au kutibu sumu ya zebaki. Sheria na harakati
zilizopo juu ya zebaki zimeshindwa kwa kiasi kikubwa sana kupunguza matumizi ya
zebaki.
Tanzania imesaidia utengenezaji wa mkataba wa kimataifa wa
kupunguza kujiweka wazi kwa zebaki duniani kote, ambao zaidi ya serikali 140
walikubaliana nao mnamo tarehe 1 Januari 2013. Mapatano ya Minamata juu ya Zebaki (The Minamata Convention on Mercury), yaliyopewa jina
la eneo la Japan lililokumbwa na janga la sumu ya zebaki takriban nusu karne
iliyopita, makubaliano yanayotarajiwa kufikiwa maazimio Oktoba eneo la karibu
na Minamata.
“Tanzania imesaidia kupatikana kwa Mapatano ya Minamata juu
ya Zebaki,” alisema Morna. “Na sasa ili kulinda azma ya watu wake na ukuwaji wa
sekta yake ya uchimbaji, inahitaji kuwa mstari wa mbele kulinda watoto wake –
kwa kuwalinda, kuwapima na kuwatibu watoto hao kwa kujiweka wazi na zebaki na
kuwaondoa katika migodi.”
Kufanya kazi katika migodi kunaivuruga elimu ya watoto.
Watoto wanaofanya kazi machimboni nyakati zingine hawahudhurii darasani au
wanaacha shule kabisa. Waalimu waliwaambia Shirika la Human Rights Watch kuwa
mahudhurio ya shuleni na ufaulu wa darasani vilishuka mara tu mgodi
uliopofunguliwa eneo la jirani. Lakini zaidi pia, vijana wengine
wanajitafutia ajira za kudumu, ikiwa ni pamoja na machimboni, kwasababu
wamekosa fursa za kujiunga na shule za sekondari au mafunzo ya ufundi stadi.
Kijana mwenye umri wa miaka15,wilaya ya Geita alivyoelezea kwa ufupi madhara ya uchimbaji madini katika maisha yake: “Ni vigumu kuchanganya uchimbaji na shule. Sipati muda wa kwenda mafundishoni (ambayo hufanyika mwishoni mwa wiki). Nawaza machimbo tu, yananichanganya….siku moja….niliugua (kwa ajili ya machimbo na kutohudhuria darasani). Nilihisi maumivu mwili mzima.”
Serikali ya Tanzania inapaswa kupanua zaidi upatikanaji wa elimu ya sekondari na mafunzo ya ufundi stadi na kuboresha ulinzi wa watoto, aseme shirika la Human Rights Watch . Serikali na wahisani wanapaswa kutoa msaada wa kifedha na kisiasa kwa mkakati mpya juu ya watoto walio katika mazingira hatarishi na kuwajumuisha yatima waishio maeneo ya migodini katika mpango wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Tanzania wa ruzuku na utoaji wa pesa kwa watu waishio katika mazingira hatarishi.
Kijana mwenye umri wa miaka15,wilaya ya Geita alivyoelezea kwa ufupi madhara ya uchimbaji madini katika maisha yake: “Ni vigumu kuchanganya uchimbaji na shule. Sipati muda wa kwenda mafundishoni (ambayo hufanyika mwishoni mwa wiki). Nawaza machimbo tu, yananichanganya….siku moja….niliugua (kwa ajili ya machimbo na kutohudhuria darasani). Nilihisi maumivu mwili mzima.”
Serikali ya Tanzania inapaswa kupanua zaidi upatikanaji wa elimu ya sekondari na mafunzo ya ufundi stadi na kuboresha ulinzi wa watoto, aseme shirika la Human Rights Watch . Serikali na wahisani wanapaswa kutoa msaada wa kifedha na kisiasa kwa mkakati mpya juu ya watoto walio katika mazingira hatarishi na kuwajumuisha yatima waishio maeneo ya migodini katika mpango wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Tanzania wa ruzuku na utoaji wa pesa kwa watu waishio katika mazingira hatarishi.
Benki ya Dunia na wahisani wengine katika sekta ya madini
wanapaswa pia kuunga mkono hatua za ukomeshwaji wa ajira kwa watoto migodini na
kupunguza kujiweka wazi kwa zebaki kwa watoto na watu wazima, aseme shirika la
Human Rights Watch . Kwa mfano, wanapaswa kuwasaidia watoto kuhama kutoka
kazini katika migodi isiyo na leseni na kuingia shuleni, na kuhakikisha kwamba
migodi mipya inayopewa leseni haitumii ajira kwa watoto. Mradi wa sasa wa dola
milioni 55 wa Benki ya Dunia kusaidia sekta ya madini hautatui tatizo la ajira
kwa watoto moja kwa moja.
Sekta ya madini ina wajibu wa kuhakikisha hainufaiki kwa
namna yoyote ile kutokana na ajira kwa watoto iliyokinyume na sheria, aseme
shirika la Human Rights Watch . Wakati huo huo wauzaji wa dhahabu waliohojiwa
na shirika la Human Rights Watch nchini Tanzania hawakuwa na utaratibu wowote
ule wa kuzuia mzunguko wa upatikani wa dhahabu iliyochimbwa na watoto.
Wauzaji wadogo wadogo mara zote hununua dhahabu moja kwa
moja kutoka machimboni na katika miji iliyo na machimbo halafu huiuza kwa
wauzaji wakubwa Tanzania. Nyakati zingine dhahabu hii hupita kwa washenga wengi
kabla haijawafikia wauzaji wakubwa wanaouza dhahabu nje ya nchi. Kwa mujibu wa
serikali ya Tanzania, wachimbaji wadogo wadogo walitengeneza takribani tani 1.6
za dhahabu mnamo mwaka 2012 – iliyokuwa na thamani ya karibu dola milioni 85.
Maeneo makubwa ambayo dhahabu ya wachimbaji wadogo wadogo wa Tanzania huelekea mara nyingi ni pamoja na nchi za Muungano wa Falme ya Kiarabu (UAE). Dhahabu pia husafirishwa kwenda Uswisi , Afrika Kusini, China na Uingereza.
Maeneo makubwa ambayo dhahabu ya wachimbaji wadogo wadogo wa Tanzania huelekea mara nyingi ni pamoja na nchi za Muungano wa Falme ya Kiarabu (UAE). Dhahabu pia husafirishwa kwenda Uswisi , Afrika Kusini, China na Uingereza.
“Iwe kwa kiwango kikubwa au kidogo, nchini Tanzania au dunia
nzima, biashara ni lazima iache matumizi haramu ya ajira kwa watoto katika
upatikanaji wa dhahabu yao,” amesema Morna. “Kwa wale wenye nguvu ya ununuzi,
wanaushawishi mkubwa kwa wauzaji wa dhahabu. Wanapaswa kuitumia kuwalinda
watoto na kuwalinda watumiaji kununua dhahabu itokanayo na ajira kwa watoto.”
Comments
Post a Comment