ASILIMIA 90 YA WATOTO WALEMAVU HAWAENDI SHULE KUTOKANA NA DHANA POTOFU KATIKA JAMII MIMI NA WEWE TUSAIDIANE KUWATETEA WALEMAVU

Serikali imeombwa kulipa kipaumbele suala la umuhimu wa makundi ya walemavu kupewa haki zao za msingi ikiwemo elimu kufuatia utafiti uliofanywa na wataalama wa kimataifa wanaohudumia walemavu wa aina tofauti nchini kubaini kuwa asilimia 98% ya makundi ya watoto wenye ulemavu hawaendi shule kwa sababu mbali mbali ikiwemo dhana potofu iliyopo miongoni mwa jamii.

 Akizungumza na mamia ya wananchi katika kijiji cha Duga kilichopo kata ya Duga wilayani Mkinga katika zoezi la kuhamisisha jamii kuwapatia haki zao za msingi walemavu  mtaalam wa kuhudumia walemavu kutoka nchini Thailand Dr,Kirsi Salo  amesema katika utafiti wao walioufanya katika mikoa mbali mbali nchini baadhi yao wamefichwa majumbani kutokana na imani haba za kishirikina  kuwa kuzaa mtoto mlemavu ni mikosi ndani ya familia na baadhi ya familia hudiriki hata kupoteza maisha yao.
Kwa upande wake kiongozi wa kanisa la kilutheri usharika wa Duga mchungaji Clementi Hongele ambaye amedai kuwa kati ya walemavu 600 waliopo wilayani Mkinga kata ya Duga ndiyo inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya walemavu na kusisitiza kuwa suala la unyanyapaa lililojengeka miongoni mwa jamii hasa kwa jamii ya wafugaji imekuwa ndio chanzo cha kuwaficha watoto wao walemavu katika vyumba maalum badala ya kuwapaleka katika shule maalum ambazo zinawajengea uwezo wa kimaisha.
Mmoja kati ya wazazi wenye watoto walemavu Bibi Mwanakombo Bakari analishukuru umoja wa makanisa kutoka nchini Finland na mashirika ya kimataifa yanayoshirikiana na kanisa la kiinjili la kilutheri (KKKT) dayaosos ya kaskazini mashariki kwa kusaidia walemavu wa kata hiyo bila kujali itikadi za kidini hatua ambayo imesaidia kuondoa dhana potofu ya unyanyapaa hasa baada ya wanavijiji kupewa elimu kuhusu athari na madhara ya kuwaficha watoto wenye ulemavu.

Comments

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU