AJIRA ZA WATOTO MIGODINI NCHINI TANZANIA ZINA ATHARI MBAYA
Shirika la Kuteteta Haki za Binadamu la Human
Rights Watch limetangaza kuwa, watoto wa maeneo ya migodi nchini Tanzania
wanakabiliwa na mazingira magumu. Ripoti
ya shirika hilo inabainisha kwamba, watoto wamekuwa wakijiingiza kwenye ajira
ya uchimbaji madini nchini Tanzania huku wengi wao wakiathirika kiafya. Aidha
ripoti ya Shirika la Kuteteta Haki za Binadamu la Human Rights Watch imesema
kuwa, kuna vitendo vya dhuluma na ukatili wa kijinsia unaofanywa dhidi ya
watoto hao wanaofanya kazi katika baadhi ya maeneo ya migodi nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadhi ya watoto hao wapo hatarini kuangukia kwenye
matatizo ya kiafya, ikiwamo mtindio wa ubongo kutokana na kemikali
zinazopatikana kwenye machimbo hayo ya madini. Idadi kubwa ya watoto hao hufanya
kazi kwenye mazingira magumu na wakati mwingine hulazimika kuingia kwenye
mapango yaliyopo chini kwa chini, kwa ajili ya kusaka madini, imebainisha
ripoti hiyo ya Human Rights Watch.
Comments
Post a Comment