UKOSEFU WA SHULE ZA WATOTO WENYE ULEMAVU WA KUSIKIA JIJINI ARUSHA WASABABISHA WATOTO 200 KUKOSA ELIMU YA MSINGI KWA KILA MWAKA.
Na Gladness Mushi, Arusha
IMEELEZWA
zaidi ya watoto 200 wenye ulemavu wa kusikia katika mkoa wa Arusha
wanashindwa kwenda mashuleni kila mwaka kutokana na ukosefu wa shule
maalumu za watoto wenye ulemavu wa kusikia lakini pia uhaba wa walimu.
Hayo
yameelezwa na Bi rafiki Msafiri ambaye ni katibu wa chama cha viziwi mkoa
wa Arusha(CHAVITA) wakati akiongea na wadau wa chama hicho kuhusiana na
mapendekezo yao kwenye mchakato wa rasimu ya katiba mpya.
Bi
Rafiki alisema kuwa idadi hiyo ya watoto wenye ulemavu wa
kusikia inatokana na changamoto mbalimbali za kijamii ambazo bado
hazijatekelezwa hali ambayo inaongeza watoto
wasiojua kusoma na kuandika kwa mkoa wa Arusha kwa visingizo kuwa ni
walemavu
Alifafanua
kuwa kwa mkoa wa Arsuha shule zenye vitengo vya watoti wenye ulamabu wa
kusikia ni chache kuhu kutokana na uchache huo
unasababisha watoto kumi tu wachukuliwe kila
mwaka tofauti na idadi ya watoto 200 wanaohitaji kujiunga na elimu ya
msingi
Aliongeza
kuwa hali hiyo ya kitaaluma sio nzuri hata kidogo kwani inachangia wimbi
kubwa sana la watoto wa mitaani ambao wanakaa
majumbani na kisha kukosa mwelekeo wa kielimu
jambo ambalo pia ni chanzo kikubwa sana cha umaskini
“kila
mwaka watoto wenye ulamavu wanakaa majumbani kwa kuwa shule ni chache
walimu wenyewe ni wachache sana vifaa navyo vipo vichache sana hivyo basi
tunaomba serikali na hata hii Rasimu ya Katiba mpya iweze kuangalia suala
hili”aliongeza Bi rafiki
Mbali
na hayo alidai kuwa ni vema kama Rasimu ya Katiba mpya pia ikaweza
kuangalia matumizi sahihi ya alama za walemavu kwani ukosefu wa alama hizo
pia unachangia sana umaskini kwenye jamii lakini pia kupuuzwa kwenye
mahitaji ya msingi
Pia alisema kuwa kama rasimu ya katiba mpya
itaweza kuwa na matumizi sahihi ya alama kwa walemavu na pia itaweka
adhabu kali kwa watendaji wa serikali ambao watapuuza alama hizo basi
jamii hiyo ya walemavu wataweza kufanya mabadiliko ya hali ya juu sana na
hivyo hata kuchangia pato la taifa.
“kwa
mfano unaweza kukuta sisi tunataarifa Fulani juu ya jambo Fulani kwa kuwa
tumeshaliona lakini tukienda mahali kama vile Polisi
tunazungushwa na hatusikilizwi ukisema uje
hata kwa vgiongozi wa Jiji, na Hospitali nao wanaona kama sisi ni
wasumbufu wakati Katiba
imeonesha kuwa tunahaki ya kuishi kama Raia
wengine”alifafanua zaidi Bi Rafiki
Comments
Post a Comment