WATOTO WA MITAANI WANAHITAJI SAUTI YAKO.
Tatizo la watoto wa mitaani na vijana wa mitaani
limekuwa ni tatizo sugu na linalozidi kuongezeka siku hadi siku. Watoto hawa
wanaishi mazingira hatarishi na wanazikosa haki zao za msingi kama vile elimu,
malezi bora na mahitaji muhimu kama chakula mavazi na malazi
Watoto hawa ndiyo wanakuwa vijana wa mitaani
wanapokuwa wakubwa, kundi hili la vijana wa mitaani limekuwa ni kundi kubwa na
lisilo na kazi yoyote ya kufanya mitaani hali inayotoa nafasi kwa vijana hawa kujihusisha
na makundi hatari ya uvutaji na utumiaji wa madawa ya kulevya na kusababisha
nguvu kazi ya jamii na taifa kwa ujumla kupotea, vijana wenyewe kushindwa kuwa
na mwelekeo na mtazamo chanya dhidi ya maisha yao ya sasa na baadaye
Hali hii ya uwepo wa watoto wa mitaani
inasababishwa na sababu nyingi zikiwemo umasikini, utengano wa familia na vifo
vinavyosababishwa na ugonjwa hatari wa UKIMWI.
HEAR MY
VOICE (HMV) inatambua na kuthamini uwepo na mchango mkubwa unaofanywa na
taasisi, mashirika ya aina zote na serikali dhidi ya tatizo hili la watoto na
vijana wa mitaani. Jitihada hizi zitasaidia sana katika kulipunguza au
kulimaliza kabisa tatizo la watoto wa mitaani, kila mmoja katika jamii akiguswa
kwa nafasi yake ni matumaini yangu ipo siku TANZANIA itawezekana bila WATOTO wa MITAANI.
Watoto wengi wa mitaani wana uwezekano wa kutumia dawa za kulevya na
kuwa waathirika wa uhalifu. Kijana aliye katikati akivuta harufu ya
gundi.
Kijana akiwa amekaa kwenye lundo la takataka. Watoto wa
mitaani mara nyingi hulala kwenye majengo mabovu ya miji mbalimbali na katika
kona za mitaa.
Comments
Post a Comment