MITAZAMO POTOFU
Changamoto wanazokabiliana nazo watoto wenye ulemavu
Watoto wenye ulemavu mara kwa mara katika maisha ya kila siku wamekuwa
wakikabiliwa na vitendo vya kubaguliwa.Wamekuwa wakitengwa na kukataliwa
kutokana na ulemavu wao
Pata nafasi ya kumfahamu mmoja wao, na kwa kupitia yeye utaifahamu duniaTakriban asilimia kumi ya idadi ya watu wote duniani ni walemavu. Ingawaje wamekuwa wakijikimu maisha yao kwa kuombaomba katika miji barani Afrika, lakini madhara wanayokabiliana nayo walemavu hao ikiwa ni pamoja na wale wasiyoona yanapuuzwa. Baadhi ya walemavu wengine wamekuwa wakifungiwa majumbani na familia zao, kwasababu wanachukuliwa kama watazitia aibu familia hizo au hata kuwachukulia kuwa ni laana kutoka kwa mizimu.
Mikataba ipo ya kuwalinda walemavu. Hata hivyo idadi kubwa ya watu hao wameendelea kukumbana na vizuizi katika jamii. Wanatengwa katika maisha ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni, na mara kwa mara wamekuwa wakinyimwa haki za kushiriki katika siasa na kuwa huru kutoa fikra zao.
Comments
Post a Comment