Baraza
la watoto wenye ulemavu kutembelea shule Katavi, Rukwa
Baraza
la watoto wenye ulemavu kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi limeanza kutekeleza
mpango wa kuwatembelea wanafunzi wenzao wasiokuwa na ulemavu katika shule za
msingi za mikoa hiyo ili kuwashirikisha juu ya mahitaji na haki sawa katika
masuala yanayohusu haki za watoto.
Mwenyekiti
wa baraza hilo bw. Abisai Joackim amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo
na hamasa juu ya elimu shirikishi watoto wenye ulemavu wanaosoma katika shule
za msingi na sekondari katika wilaya za Sumbawanga Nkasi na Mpanda.
Mkutano
wa pamoja kati ya wajumbe wa baraza hilo na wanafunzi wasiokuwa na ulemavu wa
shule ya msingi ya Kiwelu iliopo katika halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga
umeonyesha ari na nia ya kweli ya kupatikana kwa hamasa kwa jamii juu ya elimu
shirikishi.
Watoto
wenye ulemavu kutoka baraza hilo linalodhaminiwa na kanisa la Free Pentocost
Church of Tanzania-FPTC-wakiwa na nafasi ya kuwaelezea wenzao wasiokuwa na
ulemavu juu ya mahitaji na haki sawa kwa wote.
Ushiriki
wa watoto wasiokuwa na ulemavu ulikwenda sambamba na kauli yao ya kutaka
kukomeshwa kwa unyanyasaji wa aina yoyote wa kimaumbile na kutoa wito kwa jamii
kuwathamini walemavu.
Nswima
Ernest, TBC Sumbawanga.
Comments
Post a Comment