TANZANIA: MAISHA YA HATARI YA WATOTO WACHIMBA DHAHABU
Serikali, Benki ya Dunia, Wahisani Wanapaswa Kushughulikia swala la Ajira Kwa Watoto Migodini Two 13-year-old boys dig for gold ore at a small-scale mine in Mbeya Region, Tanzania. © 2013 Justin Purefoy for Human Rights Watch. Vijana wadogo wakike na wakiume wa Kitanzania wanashawishika kujiingiza katika uchimbaji wa dhahabu wakitumaini kupata maisha bora, lakini baadae wanajikuta wamekwama katika mzunguko mbaya wa hatari na kukata tamaa. Tanzania na wahisani wanahitaji kuwatoa watoto hawa katika migodi na kuwaingiza shuleni ao katika mafunzo ya ufundi stadi. Janine Morna, mtafiti wa haki za watoto wa shirika la Human Rights Watch (Dar Es Salaam) – Watoto wenye umri mdogo wa hadi miaka minane wanafanya kazi katika migodi midogo midogo ya dhahabu