MTOTO ANUSURIKA KUUAWA... WAZAZI HAKUNA MTOTO ANAYEPENDA KUZALIWA AKIWA MLEMAVU.....
BAADHI YA WATU WAMEKUWA NA MITAZAMO HASI DHIDI YA WATOTO WANAOZALIWA NA ULEMAVU WA AINA MBALIMBALI, NA HICHA NI CHANZO CHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA, HAKUNA MTOTO ANAYEPENDA KUZALIWA MLEMAVU, WALA MAMA ANAYEPENDA KUJIFUNGUA MTOTO MLEMAVU ILA YOTE NI MIPANGO YA MUNGU WETU AMBAYE NDIYE MUUMBAJI, SIO MKOSI WALA LAANA KUZAA MTOTO MLEMAVU... Mkazi wa Kawe, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Betty Mwani (25) amewaomba Watanzania na mashirika yasiyo ya kiserikali kumsaidia mahitaji mbalimbali mwanaye Saraphina Huruma Msaka (7) (pichani) ambaye ni mlemavu aliyenusurika kuuawa. Akizungumza hivi karibuni nyumbani kwa dada yake, Kawe anakoishi, Mwani alisema kwamba mwanaye alitaka kuuawa kijijini kwao kutokana na imani za baadhi ya watu kuwa katika ukoo wao mtoto kuzaliwa na ulemavu ni mkosi. Hata hivyo, Mwami alisema aliweza kuondoka na kuja jijini ambako mtoto wake anakabiliwa na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa baiskeli ya magurudumu...