WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA
Ukatili dhidi ya watoto umeongeza idadi ya watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi licha ya kuwepo juhudi za kupambana na tatizo hilo. Watoto wanaoishi katika mazingira hayo, huathirika kisaikolojia kutokana na kujiingiza katika vitendo vya matumizi ya gundi na dawa za kulevya, huku sehemu ya jamii katika ngazi ya familia na kuficha tatizo badala ya kulipeleka kwenye vyombo vya dola. Wanafanya hivyo kwa maelezo kuwa wanaogopa aibu, matokeo yake kuna ongezeko la watoto wa mtaani, baadhi ambao bado wapo chini ya matunzo ya wazazi wao, lakini wanajiingiza katika tabia ya kuomba fedha na wanaonekana mitaani katika miji mbali mbali nchini. Ukatili unafanyika dhidi ya watoto kuanzia ngazi ya familia na ndugu wa karibu kwa kumbaka au kumlawiti mtoto anyeishi nao. Sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009, inalenga kurekebisha na kuimarisha sheria zote zihusuzo watoto, kuainisha haki, kukuza na kulinda maslahi bora ya watoto kwa mujibu wa sheria. Kuna uwezekano wa kul
maisha ya hawa watoto ni magumu sana
ReplyDeletehasa mateso wayapato wakati wa usiku
ReplyDelete