PATA ELIMU TUMIKIA KWA HURUMA. (SEKOMU)

Mchungaji Chrispus Kanju Mkuu wa Idara ya Diakonia Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili ERENTE Lushoto Tanga ikiwa ni sehemu ya huduma ya idara yake.

Mlezi wa watoto wenye ulemavu wa akili katika kituo cha ERENTE akifafanua jambo mbele ya wanachuo wa SEKOMU walipokitembelea kituo hicho katika moja ya ziara zao katika vituo mbalimbali vinavyolea watoto wenye mahitaji maalumu.
Baadhi ya watoto katika kituo cha ERENTE wakiwa katika picha ya pamoja na Wanachou wa SEKOMU na Mchungaji Kanju.

Hezron Cherehani akiwa na mmoja wa watoto wenye ulemavu wa viungo katika kituo cha ERENTE.
                                                                    Burudani.......

NI WITO WANGU KWA WAHITIMU WOTE SEKOMU 2013, HAWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WANATUTEGEMEA SISI, ELIMU TULIYOIPATA TUKAITUMIE KUWASAIDIA. SISI NDIO SAUTI ZAO NA KATIKA KUWATIMIZIA MAHITAJI YAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WATAJISIKIA FARAJA NA WATATAMBUA KUWA WAO PIA NI SEHEMU YA JAMII INAYOWAZUNGUKA. 
BADO KUNA MITAZAMO HASI KWA JAMII DHIDI YA HAWA WATOTO TENA KWA KIWANGO KIKUBWA SANA, KWA TAALUMA TULIYOIPATA CHUONI SEKOMU TUKAITUMIE KUIELIMISHA JAMII JUU YA ULEMAVU WA AINA ZOTE, ULEMAVU WA AKILI, ULEMAVU WA VIUNGO, ULEMAVU WA NGOZI, KUTOKUSIKIA NA KUTOKUONA, KWA KUFANYA HIVYO TUTAKUWA MABALOZI WAZURI WA HAWA WATOTO NA TAALUMA YETU PIA. 
SIMAMA IMARA, SEMA KWA SAUTI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WANAITEGEMEA SAUTI YAKO.!!!!!!
MUNGU IBARIKI SEKOMU, MUNGU IBARIKI TANZANIA.


Comments

  1. safi sana kaka James

    ReplyDelete
  2. Nashukuru ndg ni jukumu letu sote.

    ReplyDelete
  3. HONGERENI SANA, JAMII INAWAHITAJI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana, tupo tayari kuitumikia jamii yetu.

      Delete
  4. Elimu maalumu kwa tanzania inafundishwa SEKOMU tu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. SEKOMU ni chuo kinachotoa bachelor na masters katika elimu maalumu, ni chuo pekee kwa Afrika Mashariki kinachotoa masters katika elimu maalumu. Karibu sana SEKOMU.

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU