HAKUNA SABABU YA KUWAFICHA WATOTO WENYE ULEMAVU, WANA HAKI SAWA KAMA WATOTO WASIO NA ULEMAVU.

WAZAZI BADO WAENDELEA NA DHANA YA KUWAFICHA WATOTO WALEMAVU MAJUMBANI MKOANI MBEYA

Na Ester Macha, Mbeya.
 LICHA ya serikali kutoa elimu kwa jamii,wazazi na walezi kuacha kuwaficha majumbani watoto wenye ulemavu na badala yake wawapeleke shule hali imekuwa tofauti mkoani Mbeya ambapo baadhi ya wazazi bado wanawaficha watoto wao majumbani na wanapofuatiliwa wanasema hawana watoto wa aina hiyo.
 Aidha ikiwa wanawake na wanaharakati nchini wakiwa katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  kwa wanawake,watoto na walemavu  hali bado tete ya ukatili,unyanyapaa  na kukosa haki za msingi kwa makundi maalum hivyo  kunahitajika nguvu ya ziada  kukabiliana na hali hiyo.
 Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo,Mwalimu Bi.Suzana Kidily katika mahafali ya kwanza ya wanafunzi wa kitengo maalum katika shule ya msingi Mwenge,jijini Mbeya ambapo wanafunzi tisa wakiwemo wa kike wanne na wakiume watano walihitimu.
Bi.Kidily alisema kuwa kunahitajika kazi ya ziada ya kuendelea kuielimisha jamii kuhusu haki za mtoto mwenye ulemavu ili wazazi na walezi waondokane na dhana potofu ya kwamba hawastahili kupata huduma muhimu za kijamii sanjari na kusoma,kutibiwa,kucheza na kuongea na wenzao.
Alitoa mara kadhaa baada ya kupokea taarifa za uwepo wa watoto wenye ulemavu katika baadhi ya nyumba wamekuwa wakifanya ufuatiliaji na kuwasiliana na wakuu wa familia husika lakini katika hatua ya kushangaza wanakataa kuishi na watoto wa aina hiyo na inafikia hatua ya kujibu kwa jazba wanapoona wanaendelea kuwabana kwa maswali ambayo yanayonesha dhahiri kufichua ukweli.
Hata hivyo ametoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa,vitongoji,Kijiji na Kata kushirikiana na walimu wa vitengo maalum katika kutoa taarifa zitakazosaidia kuwafichua na kuwasaidia watoto wenye ulemavu wanaonyimwa haki zao za msingi kwa sababu ya wazazi ama walezi kuona aibu ama kutofahamu kwamba watoto wenye ulemavu ni binadamu kama wa livyo watoto wengine.
Kwa upande wake Mwalimu Maalum kutoka shule ya Msingi Nsalaga,Bi.Nely Elisha alisema  kuwa jamii bado ina mtazamo hasi wa walimu maalum wanaowafundisha watoto wenye ulemavu wa akili kutokana na kuwaona kama walimu nao ni walemavu kama wanafunzi wanaowafundisha na hivyo si chochote,wamechanganyikiwa,hawafai na hata mawazo yao kutothaminika katika jamii wanazoishi.

Comments

  1. HILO NI TATIZO HASA KWA JAMII AMBAZO WANA MTAZAMO HASI JUU YA ULEMAVU.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WATOTO WA MITAANI NA JINSI YA KUWASAIDIA

AYA ZA BIBLIA KUHUSU WATU WENYE ULEMAVU

TUWAKUMBUKE WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KAMA KUNDI MAALUM KATIKA JAMII ZETU