David Mangare: Yatima aliyethubutu Na Dismas Lyassa, Mwananchi SHARE THIS STORY Tajiri maarufu Duniani, Bill Gates wakati fulani amewahi kunukuliwa akisema kinachowasumbua watu wengi kutofanikiwa ni wao wenyewe kutopenda kuthubutu. Siku moja akiwa kwenye chuo kimoja akitoa nasaha zake, Bill Gates alisema “Mwanafunzi niliyesoma nae ambaye alikuwa akinishinda kwenye mitihani mingi, sasa hivi nimemuajiri, ni fundi wangu, alinishinda elimu darasani, mimi leo namshinda utajiri, amekuwa kati ya maelfu ya wafanyakazi ninaowalipa mshahara”. Anachosema Bill Gates ni ukweli kuwa kusoma au kutosoma, ama kuzaliwa familia tajiri au maskini, sio tiketi kwamba unaweza kuwa tajiri au la. Siri ya ushindi Kinachoweza kumsaidia mtu kuwa na maisha yenye mafanikio ni uwezo wake katika kuthubutu kufanya mambo, hasa pale anapoyafanya kwa ustadi huleta tija zaidi. Mtafiti wa masuala ya saikolojia, Norman Vincent Peale wa Marekani anasema katika kitabu chake ...