NENO LANGU.
......WAACHENI
WATOTO WADOGO WAJE KWANGU MAANA UFALME WA MUNGU NI WAO. TUWASAIDIE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU, NI WATOTO WETU
NA WADOGO ZETU......
Kila mtu ana historia
yake ama mbaya au nzuri ya enzi za utoto wake wapo ambao wakikumbuka nyuma
wanalia na kuichukia dunia maana walikosa tumaini na faraja toka utotoni mwao. Leo
hii sisi tuliokwisha ona angalau mwanga katika hii dunia ni vyema tukawa
tumaini au faraja nzuri kwa watoto wote wenye mahitaji maalumu katika jamii, tukiwasaidia kuanzia malezi bora, elimu
bora lakini pia kunyanyua na kuvumbua vipaji vyao ili kuvikuza waje kuwa zao
jema ukubwani, wasije wakalia na kuichukia dunia kama wengine, ni jukumu letu
kama jamii, kujali, kuthamini na kutambua wajibu wetu kwa hawa watoto. Kuna makundi
mbalimbali ya watoto ambao bila kujitoa kwetu kwa ajili yao ni sawa na kuundaa
kizazi ambacho kwao furaha na upendo vitakuwa ni vitu vya kuvisikia kwa
wengine, pia ni sawa na kuandaa kizazi chenye chuki na hasira na matokeo yake
ni kujiingiza katika vitendo visivyo vya kiungwana.
MIMI, WEWE NA YULE
TUWE SEHEMU YA FURAHA KWA HAWA WATOTO.
Comments
Post a Comment