NI WAJIBU WETU.
JAMII IWAJIBIKE KUWASAIDIA WATOTO WA MITAANI, YATIMA....
Kitanda usichokilalia, huwezi kujua 
kunguni wake, shida na mateso wanayoyapata watoto waishio katika 
mazingira hatarishi na wale wa mitaani ni vigumu kuyaeleza. Watoto hawa 
hawajui leo au kesho watakula nini, hakuna anayehangaika kuwatafutia 
chakula, wanapolala na njaa hakuna wa kumlilia na wakiumwa hakuna wa 
kumweleza hivyo huendelea na maisha yao hadi wanapopata nafuu au kupona 
kabisa.
     Ukweli ni kwamba, watoto hawa 
hujisikia wapweke kutokana na jamii kubwa kuwakataa na kuwaweka katika 
fungu tofauti. Jambo la kusikitisha ni idadi kubwa ya watoto hawa umri wao 
unaanzia miaka miwili hadi kumi ambao kimsingi hawajui kujitegemea, njaa 
ikiuma wanalia tu na kushindwa kujieleza. Kitanda chao ni barabarani na 
wengine mitaroni, baridi yote ya usiku na jua la mchana ni lao ,hawajui 
kubadilisha nguo, zile walizovaa wiki iliyopita hadi leo hazijatoka 
mwilini,  Tumezoea kuwaona watoto wenye wazazi wakitoka nyumbani 
asubuhi na kurudi majumbani mwao jioni. Watoto yatima na wanaoishi 
katika mazingira hatarishi hawana pa kwenda, popote wanalala.  Jamii 
imesahau kuwa watoto hawa ni sawa na wao, wanasikia njaa, baridi na 
maumivu sawa na wenzao lakini nani anashughulika nao?
    Watoto hawa hawakuchagua kuwa 
yatima na kuishi mitaani, hawakuchagua kufiwa na wazazi wao, wamejikuta 
wapo mitaani na hawana la kufanya kama watoto wetu wanavyojikuta wakiwa 
mikononi mwetu na wanapata kila kitu. Waswahili wanasema, kinga ni bora 
kiliko tiba. Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs na yale ya kimataifa 
kama UNICEF na Serikali ,wanashughulikia tatizo la watoto hawa wakiwa 
tayari mitaani, jambo ambalo ni sahihi na la msingi, ni bora nguvu inayotumika kuwasaidia watoto 
hawa ingepaswa kuelekezwa kwenye kinga ili kutibu tatizo hilo 
kabisa. Sababu moja wapo inayochangia ongezeko la yatima na watoto wa 
mitaani ni migogoro isiyokwisha  katika ndoa na umasikini uliokithiri
      Hatua za haraka zinahitajika 
ili kupunguza au kumaliza tatizo la watoto wa mitaani  na yatima kwa 
kuwaunganisha na walezi pamoja na ndugu zao ambao tunaamini wapi.
      Umefika wakati wa serikali 
kuratibu nguvu za NGOs kwa kuhakikisha mashirika hayo na jamii wanachukua hatua stahiki  kuhakikisha tatizo hilo nchini 
linakwisha... 
MUNGU IBARIKI TANZANIA... MUNGU IBARIKI AFRIKA.



dunia haina usawa, wengine wana maisha mazuri ili hali wengine mlo mmoja kwao ni taabu
ReplyDeleteNi kweli kabisa na kitu kikubwa kinachosababisha yaho yote in UBINAFISI.
DeleteNi kweli kabisa na kitu kikubwa kinachosababisha hayo yote in UBINAFISI.
Deletemtu anakuwa na gari 20 za kutembelea, anakutana na watoto wa mitaani hata kuguswa tu na hali waliyonayo wale watoto kwake haipo.
DeleteInabidi roho mtakatifu atuguse katika hili.
Delete